Rekodi zinaibeba klabu ya Manchester United dhidi ya Manchester City katika uwanja wa Etihad ambapo ni uwanja wa nyumbani wa klabu ya Manchester City.

rekodiMchezo kati ya vilabu hivo vinavyotoka katika jiji moja utapigwa kesho siku ya jumapili oktoba 2 huku klabu ya Manchester City ikipewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo,Hii ni kutokana na kiwango kikubwa walichokionesha kwenye mechi kadhaa zilizopita huku Man United wao licha ya kushinda michezo minne mfululizo ya ligi hiyo bado hawaoewi nafasi kubwa katika mchezo huo wa dabi ya Manchester.

Tukirudi kwenye rekodi klabu ya Manchester United inaonekana kua mbabe wa City siku za hivi karibuni kwani kwenye michezo nane ya mwisho walipokutana katika dimba la Etihad United wameshinda michezo mitano huku wakipoteza miwili na kusuluhu mmoja hii inaonesha kwa kiwango gani klabu ya United licha ya kutokua vizuri miaka ya karibuni lakini wamekua wakipata matokeo mazuri katika uwanja wa nyumbani wa City na ni rekodi nzuri kwao kuelekea mchezo hapo kesho.

rekodiKuelekea mchezo huo wa dabi hapo kesho vita kubwa inayotazamiwa ni kati ya mshambuliaji hatari wa City Earling Haaland dhidi ya beki katili wa klabu ya United Lisandro Martinez kwani vita yao itakua ni muendelezo baada ya kukutana na katika vilabu vyao vya awali Haaland akiwa Dortmund ya nchini Ujerumani na Martinez akiwa Ajax ya nchini Uholanzi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa