Chelsea Wapo Mbele Kumsajili Nkunku Baada ya Vipimo

Chelsea baada ya kufanya vipimo vya siri na mchezaji wa Rb Leipzig Christophe Nkunku na kupiga hatua mbele zaidi kuwazidi wapinzani wao kwenye usajili wa mchezaji huyo anayecheza eneo la ushambuliaji.

 

Chelsea Wapo Mbele Kumsajili Nkunku Baada ya Vipimo

 

Kulingana na The Telegraph, The Blues walifanya vipimo vya siri vya matibabu na mchezaji huyo ambae ana umri wa miaka 24 katika majira ya joto. Mchezaji huyo anakipiga katika ligi ya Ujerumani.

Nkunku ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni ya Milioni 52.5 katika mkataba wake na maslahi mengi yanatarajiwa kuja msimu ujao wa joto. Baada ya kampeni nzuri ya 2021-22 iliyomfanya aifungie Leipzig mara 35, ameanza msimu huu kwa mtindo mzuri na kushinda mabao sita katika michezo 11.

 

Chelsea Wapo Mbele Kumsajili Nkunku Baada ya Vipimo

Na Chelsea wanamhitaji  sana Mfaransa huyo kwani bado kuna shida ya ufungaji magoli, hivyo akitua pale Stamford Bridge kwa Graham Potter anaweza kuongeza kitu katika klabu hiyo ya London.

Nkunku bado anahitaji kufanyiwa vipimo kamili vya matibabu mnamo 2023, ingawa masharti ya kibinafsi yameripotiwa kukubaliwa kati yake na klabu hiyo ya The Blues.Lakini hilo halitavizuia vilabu vingine kujaribu kumtaka mshambuliaji huyo ambaye ana ubora wake, ikiwa ataendelea nao.

Ripoti hiyo inaongeza kuwa Chelsea wamezungumza na Meneja mpya Graham Potter kuhusu uhamisho huo, ambapo kocha huyo amesema kwamba hawezi kuujadili uhamisho huo, hawezi kuongelea wachezaji wengine. Hivyo hana cha kusema.

Chelsea Wapo Mbele Kumsajili Nkunku Baada ya Vipimo

Acha ujumbe