Richarlison Akasirishwa Kutokana na Kukosa mda wa Kucheza

Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayekipiga klabu ya Tottenham Hotspurs Richarlison ametema nyongo baada ya klabu yake kutupwa nje ya michuano ya ulaya usiku wa jana na kulaumu kutokana na kutokupata mda wa kucheza.

Mshambuliaji Richarlison alionesha kutokufurahishwa na dakika ambazo anapewa ndani ya klabu hiyo baada ya mchezo wa jana kumalizika dhidi yao na klabu ya klabu ya Ac Milan, Baada ya mchezo mshambuliaji huyo alionesha kukasirishwa sana na kitendo cha kuwekwa nje.RicharlisonKlabu ya Ac Milan walifanikiwa kuitupa nje ya michuano ya ulaya klabu ya Tottenham Hostspurs hapo jana baada ya mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya bila kufungana, Mchezo wa awali ulimalizika kwa klabu ya Ac Milan kushinda bao moja kwa bila na kuweza kufuzu hatua ya robo fainali.

Mshmbuliaji Richarlison anaona kama amesalitiwa na kocha wa klabu hiyo Antonio Conte baad ya kutokupewa mda wa kutosha wa kucheza, Mshambuliaji huyo anasema alianza kwa kucheza vizuri ndani ya klabu hiyo lakini ghafla anashangaa ameanza kuwekwa benchi jambo ambalo limemshangaza.RicharlisonMshambuliaji huyo amesema aliuliza kwa kocha Conte kwanini hapati nafasi ya kucheza lakini hakupewa majibu sahihi, Lakini yeye anaamini anastahili dakika za kucheza kwani anajituma na kufanya mazoezi kwa bidiii hivo anapokua anawekwa nje sio jambo ambalo linampendeza sana yeye.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.