Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Richarlison amesema maumivu aliyoyapata baada ya timu ya taifa ya Brazil kutolewa kwenye kombe la dunia ni zaidi ya kupoteza ndugu.
Timu ya taifa ya Brazil ilitolewa kwenye fainali za kombe la dunia nchini Qatar katika hatua ya robo fainali dhidi ya timu ya taifa ya Croatia. Kitu ambacho mshambuliaji Richarlison anaona lilikua jambo gumu sana kwake kuliko hata kupoteza moja ya mtu katika familia yake.
Mshambuliaji huyo anasema ni jambo gumu zaidi kulipitia kwani imekua ngumu kupona maumivu hayo, Kwani maumivu hayo anayopata pale ambapo anakua anapitia mitandao ya kijamii na kuona baadhi ya video mbalimbali zinazohusisha mchezo waliotolewa hua bado zinampa huzuni kubwa.
Richarlison anasema inabidi akubali kusonga mbele licha ya maumivu makali ambayo amekua akiyapata, Lakini akisisitiza umri wake bado ni mdogo hivo ana michuano miwili ya kombe la dunia au mmoja hivo ataendelea kupambana kuhakikisha anashinda taji hilo na Brazil.
Mshambuliaji Richarlison ambaye alimaliza kama mfungaji bora wa timu ya taifa ya Brazil kwenye michuano hiyo akiwa na magoli matatu amesema lengo la timu yao ilikua kumaliza kama mabingwa, Lakini pia alifurahishwa na yeye kushinda bao bora la michuano hiyo.

