Conte Ataka Wakurugenzi wa Michezo Wazungumze na Wanahabari

Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs Antonio Conte amesema kua wakurugenzi wa michezo wanapaswa kuhojiwa na wanahabari sio kila wakati makocha tu.

Kocha Antonio Conte amesema hafurahishwi na mfumo wa ligi kuu ya Uingereza kua kila wakati makocha ndio wanaohojiwa kwenye vyombo vya habari huku yeye akitaka hadi wakurugenzi wa michezo wawe wanahojiwa kwenye vyombo vya habari.conteKocha huyo aliyazungumza hayo baada ya kupoteza mchezo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa nyumbani kwao dhidi ya vinara wa ligi klabu ya soka ya Arsenal kwa mabao mawili, Na kuifanya klabu hiyo kuendelea kusalia nje ya nafasi nne za juu kwenye ligi hiyo.

Kocha Conte amesema nchini kwao Italia wakurugenzi wa michezo nao wanapata fursa ya kuhojiwa na wanahabari tofauti na nchini Uingereza, Kocha huyo anaamini hiyo itawasaidia makocha kuepuka maswali ambayo muda mwingine yanakua hayawahusu makocha.conteKocha Antonio Conte anasema anaamini kua endapo wakurugenzi a michezo watapewa nafasi ya kuongea na wanahabari basi watatoa maelezo ambayo yatawasaidia makocha kuepuka baadhi ya lawama amabazo wamekua wakitupiwa mara kwa mara.

Acha ujumbe