Kocha wa muda wa klabu ya Watford Roy Hodgson amewataka wachezaji wa timu hiyo wajitoe kwa klabu hiyo ambayo iko chini ya msimamo katika ligi kuu ya Uingereza ili waweze kuisaidia timu kubaki kwenye ligi kwa msimu ujao.

Kwenye mkutano wake wa kwanza baada ya kutambulishwa kwenye hiyo, kocha huyo mwenye miaka 74 alisema kuwa anaami kikosi chake kina uwezo wa kutosha kuweza kupigania nafasi ya kuweza kubaki kwenye ligi hiyo, lakini yeye na msaidizi wake Ray Lewington watajuwa nguzo kuweza kuwasaidia wachezaji waweze kufanya vizuri.

Roy Hodgson
Roy Hodgson

Roy Hodgson alipokuwa anahojiwa na mtandao wa klabu ya hiyo alinukuliwa akisema:-

Nakubaliana na klabu kuwa kuna kundi kubwa la wachezaji wazuri hapa, lakini inabidi wawe na mawazo ya kuweza kuyabadilisha na kuwa vitendo kwa kujito.

“Hakuna mchezo mwepesi kwenye ligi kuu ya Uingereza na kama wanataka kubaki itabidi wawe wasikivu kwa kile tunachowaambia na kkuweza kufanya vizuri ili kuweza kupata pointi tunazohitaji.”

Kocha huyo wa zamani Uingereza na Crystal Palace amekubali kuwa changamoto iliyo mbele yake ni kubwa lakini ana imani kuwa kuna michezo ya kutosha kuweza kumbakisha kwenye ligi hiyo.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa