Kocha wa timu ya taifa ya Malawi Mario Marinica amewakosoa waandaji wa michuano hiyo kutokana na huduma mbovu walizokuwa wanapatiwa timu ndogo kulinganisha na timu kubwa kwenye mashindano hayo.
Wachezaji wa Malawi walilamika kuwa huduma walizokuwa wanapewa katika hoteli waliyofikia kuwa baadhi ya huduma ambazo walikuwa wanafanya wenyewe ikiwemo kufua nguo zao za ndani na kutafuta sehemu ya kuanika.
Kocha wa timu ya taifa ya Malawi mwenye miaka 57 Mario Marinica aliweka wazi kuwa timu yake ilihitajika kujifulia nguo zao wao wenyewe kwenye mashindano hayo huku timu kubwa wakiwa wanapatiwa huduma nzuri.
“Huwezi kumuona saido mane akijifulia nguo zake za ndani na kuzianika nje, gambia nao walikuwa na tatizo sawa, na kunatofauto wa huduma hapa, timu zinahudumiwa tofauti.
“Tunazungumzia juhusu yaliyopo, tunataka kuwepo na umoja wa timu ndogo, timu ndogo zinafanya vitu vizur, lakini linapokuja swala la hatua inayofuata, watu hawataki sisi tucheze dhidi ya Cape Verde na sio Senegal kucheza na Morocco.
“Maswali ya kujiuliza; kwanini hayo yanatokea kwetu tu, kwa nini ni kwa timu ndogo, kwanin Comoro, Gambia na sisi.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.