Taarifa za ndani zinaeleza klabu ya Simba Sports imemalizana rasmi na straika la magoli kutoka kwa mabingwa wa Uganda Vipers United Cesar Lobi Manzoki. Klabu ya Simba imekubali kutoa kiasi cha dola laki moja ambayo ni sawa na milioni mia mbili thelathini na tatu za kitanzania.

Dili hii imechukua muda mrefu kutokana na kutokuelewana baina ya mshambuliaji huyo raia wa Congo na klabu yake ya Vipers. Mwanzo klabu ya Simba walielezwa mchezaji huyo amebakiza mkataba wa miezi miwili na klabu yake hiyo lakini baadae klabu ilieleza wana mkataba wa miaka miwili na mchezaji huyo na kuhitaji kiasi cha dola laki moja ili kumuachia mchezaji huyo.

Manzoki, Manzoki ni Mnyamaa., Meridianbet

Kitu ambacho kiliwapa wakati mgumu viongozi wa Simba kutoa kiasi hicho cha pesa kwa mchezaji ambae amebakiza mkataba wa miezi miwili kama ambavyo mchezaji na uongozi wake walidai.

Dili hili ambalo limekua na mvutano mkubwa kwa zaidi ya miezi miwili wa pande mbili upande wa mchezaji na klabu yake pamoja na Simba na Vipers. Pia inaelezwa wapinzani wa Simba watani zao Yanga walituma ofa ya kumuhitaji mchezaji huyo. Lakini hatua ya mwisho inaelezwa Simba wamekubali kutoa kiasi hicho cha pesa klabu ya Vipers walichohitaji ili kupata saini ya  nyota huyo raia wa Uganda fundi wa kuchana nyavu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa