Antonio Rudiger amethibitisha kwamba atajiunga na Real Madrid mkataba wake na Chelsea utakapomalizika mwishoni mwa mwezi huu.

“Ninajivunia kutangaza kwamba nitajiunga na Real Madrid. Nina furaha kubwa kwa changamoto zote zilizo mbele yangu na nina hamu kubwa ya kucheza mchezo wangu wa kwanza kwa klabu hii kubwa.” – Antonio Rudiger

Rudiger Athibitisha Kuhamia Real Madrid!
Antonio Rudiger

Madrid walishinda La Liga na Ligi ya Mabingwa. Wana Nia ya kushinda tena, kuwa na timu yenye nguvu zaidi kwa msimu wa 22/23. Hivyo wanahitaji umakini mkubwakatika dirisha la usajili, Rudiger ni mpango mzuri kwao.

Beki huyo wa kati wa Ujerumani amekuwa sehemu muhimu ya timu ya Thomas Tuchel tangu aanze kuinoa Stamford Bridge. Alikuwa mchezaji muhimu sana Chelsea iliposhinda Ligi ya Mabingwa msimu wa 2020/21, ilipoifunga Manchester City kwenye fainali huko Porto.

Rudiger, 29, ameichezea Chelsea mechi 203 tangu alipojiunga na klabu hiyo msimu wa joto wa 2017. Amefunga mabao 12 na kutoa asisti saba na pia ameichezea timu ya taifa ya Ujerumani mara 50, ambayo amefunga nayo mabao mawili.


 

SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa