Klabu kubwa nchini Tanzania Simba Sports Club imeanza kampeni ya kuwataka wanachama wake kuanza kuichangia klabu hiyo na kuipa jina kampeni hiyo “NANI ZAIDI? CHANGIA SIMBA”

Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa nndani ya klabu ya Simba kuna mpasuko wa kutokuelewana viungozi wa ngazi za juu, na baadhi wakimshutumu mkurugenzi mwendeshaji wa klabu hiyo Barbra Gonzalez kuwa anadharau na yeye ndio chanzo cha migogoro kwenye klabu hiyo.Simba

Kuna kampeni imeanzishwa na baadhi ya mashabiki huku kukiwa na tetesi kuwa kuna viongozi ndio wanaongoza kampeni hiyo, kutaka mkurugenzi wa klabu hiyo, Barbra Gonzalez aachie ngazi au bodi ya klabu hiyo imfukuze.

Simba awali ilipeleka bakuli kwa wanachama wake kwa ajiri ya kuchangia ujenzi wa uwanja huo, huku rais wa heshima wa klabu Mohamed Dewji almaarufu kama MO alichangia  shilingi 2Bilioni, ambazo kwa sasa baadhi ya mashabiki wameanza kuhoji zipo wapi na zimefanya kazi gani.

Pia inasemeka kuwa kuna ukata mkubwa kwa sasandani ya klabu hiyo, huku tetesi zikisema kuwa wachezaji wa Simba wanakaribia miezi mitatu hawajalipwa mishahara yao, ambapo hakuna aliyethibitisha hilli na kubaki kuwa ni tetesi tu na habari za vijiweni.

Simba msimu huu hawajafanikiwa kuondoka na kombe lolote, mpaka sasa na hakuna matumaini ya kupata kombe lolote, huku kukiwa na taarifa kuwa kuna wachezaji nane wanakwenda kuacha msimu huu, baada ya kumfungashia vilago kocha wa klabu hiyo Pablo Franco.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa