Rungu Linamnyemelea Lacazette!

Imedaiwa kuwa klabu ya soka ya Arsenal imeapa kumpa adhabu kali mchezaji mshambuliaji wao matata, Alexandre Lacazette! Hii ni mara baada ya kuvuja kwa taarifa kuwa staa huyo ambaye ni mzaliwa wa nchini Ufaransa alionekana akivuta gesi ya Nitrous Oxide ambayo ni maarufu kama ‘Laughing Gas’ iliyokuwa imejazwa ndani ya puto alilokuwa nalo.

kwa mujibu wa gG=azeti la Daily Star la nchini Uingereza lililochapisha makala zenye picha zilizoonesha Lacazette akiwa na puto lenye gesi hiyo mdomoni mwake. Baadaye, mchezaji huyo wa zamani wa Olympique Lyon, Ufaransa aliwatumia wanasoka wenzake wa Arsenal video iliyochukuliwa akivuta gesi hiyo kupitia mitandao yao ya kijamii.

Ingawa msemaji wa Arsenal ameshikilia kwamba tukio hilo ni suala kibinafsi litakaloshughulikiwa na klabu katika kiwango cha ndani kwa ndani, huenda Lacazette akapata adhabu kali.

Kwa sasa ni juma moja pekee limepita tangu Lacazette awe mmoja kati ya  wachezaji wengine wa Arsenal waliovunja kanuni mpya za afya zinazodhibiti maambukizi zaidi ya virusi vya Corona. Lacazette ambaye ana umri wa miaka 28 kwa sasa alionekana akiwa karibu sana na mwanamume mmoja aliyekuwa akimuoshea gari lake jijini London!

Kwa kufanya jambo hilo akawa amevunja kanuni inayotaka mtu kusimama ama kukaa umbali wa hadi mita mbili kati yake na mwingine wa jirani yake. Tusubiri kuona itakavyokuwa.

28 Komentara

    Vituko hivi vya wachezaji ambao sisi tunawaita professional players.

    Jibu

    Ni lazima awajibikie adhabu yake so akae asubirie itakavyoamuliwa

    Jibu

    Sheria ifatwe

    Jibu

    Haya marungu msimu huu yamekua kama fasheni sasa maana kila kukicha tunapata habari tofauti au wanatafuta kiki??, sema nao arsenali washamchoka lakazet maana kuna tetesi toka mwanzo za kuuzwa kwke

    Jibu

    Anastahili adhabu

    Jibu

    Sheria na haki itendekeh Asante meridian kwa update

    Jibu

    Sheria ifuate mkondo wake thanks meridian kwa update

    Jibu

    gud newz

    Jibu

    Ulaya wana sheria nyingi na kali huku kwetu wachezaji unapishana nae bar au kwenye ndondo akivuta bangi

    Jibu

    acha apate adhabu ukijifanya mjuaji faida yake ndo iyo

    Jibu

    Anastahili adhabu ili iwefundisho kwa wengine

    Jibu

    Adhabu kali ichukuliwe dhidi yake

    Jibu

    Wenzetu wanafuatilia sana aisee

    Jibu

    Atakuwa ameonewa

    Jibu

    Ni lazima mchezaji wa kulipwa kuheshimu taratibu zilizowekwa na Club kulinda hadhi yako na Club unayotumikia. Wacha akutane na rungu la Club.

    Jibu

    Ni kweli ukikosea lazima upewe adhabu

    Jibu

    Jamaa huwa anabahati mbaya sana#Meridianbettz

    Jibu

    Sheria ifatwe hanastaili adhabu
    #meridianbettz

    Jibu

    Duuh pole yake

    Jibu

    adhabu lazima ili iwe funzo kwa wengine

    Jibu

    Kweli anastahili adhabu

    Jibu

    Ninlazma afate Sheria na misingi ya club inasemaje la sivyo anastahili adhabu

    Jibu

    Mmh majanga.

    Jibu

    Duuh!ana shutuma nzinto sana inabidi sheria ifwate mkondo wake kama kavunja kanuni.

    Jibu

    Asanteni meridianbet habari za mchezo hapahapa

    Jibu

    Adhabu inamuhusu

    Jibu

    Habari mjema

    Jibu

    Apate onyo ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine pia

    Jibu

Acha ujumbe