Sajili Zinazosumbua 2018/19

Wakati mwingine kufanya usajili ni zaidi ya kucheza kamari. Hii hutokana na pale klabu inaponunua mchezaji halafu anashindwa kuendana na mifumo ya timu au akashindwa kuendana na vuguvugu la ligi husika. Haya yote huwa ni mambo ya kawaida kwenye ligi husika. Leo tunakuletea wale tunaoona wanafanya vizuri katika ligi walizosajiliwa msimu huu:

Issa Diop, bado yupo katika umri unaoshawishi kuendelea kushuhudia makubwa zaidi kutoka kwake. Katika miaka yake 22 amekuwa nguzo ndani ya kikosi cha West Ham msimu huu. Raia huyo wa Ufaransa amekuwa chachu ya mafanikio kikosini hapo na anaimarisha safu yao ya ulinzi kwa kiwango kikubwa.

Raul Jimenez, majina kama haya yanapotajwa yanawapa hasira baadhi ya mashabiki wa United, hilo linatokana na namna kikosi cha timu hiyo kinavyosumbua timu kubwa kama hizo. Pamoja na hilo wamekuwa ni daraja la mafanikio kwa klabu hiyo ya  Wolverhampton Wanderers ambayo haina kipindi kirefu kwenye ligi hiyo.

Joao Moutinho, raia huyo wa Ureno amekuwa nguzo ya mafanikio pia katika kikosi hicho cha Wolves. Akiwa na miaka 32 kwa sasa amekuwa akiwapa mashabiki wa kikosi hicho kile wanakitaka kwa kuwapa matokeo mazuri kwenye mechi ngumu. Ameichezea klabu yake mechi 114 kwa kipindi kizima alianza kuitumikia akiwa na miaka 14.

Fabinho, raia huyo wa Brazil kwa kipindi ambacho amepata kushiriki kucheza soka lake ameonesha makali ya kwanini aaminiwe kuwa kiungo mkabaji ndani ya timu yake hiyo. Hilo linatokana na aina yake ya uchezaji tangu alipokuwa Monaco. Liverpool hawapo nyuma kumuweka ili aweze kuwahudumia kwa uchezaji huo.

Lucas Torreira, hapa tunaweza kusema Arsenal waliona vyema. Ni kutokana na uwezo wa nyota huyo anaouonesha kikosini hapo. Walimnasa nyota huyo kutoka Sampdoria na kwa sasa anatoa huduma kwenye kikosi chao cha kwanza kama ilivyo ada kwa wachezaji wa aina yake. Amepata nafasi ya kuanza michezo mingi ya klabu hiyo tangu asajiliwe kikosini hapo.

Rui Patricio, mlinzi chaguo la kwanza kwenye kikosi cha taifa cha Ureno akiwa na uimara unaoifanya timu hiyo kuonekana bora sana. Sio upande huo tu pia akiweza kufanya vizuri na klabu yake ya Wolves ambayo imekuwa mwiba sana kwenye ligi. Uwepo wake ni chachu kubwa ya mafanikio kikosini hapo na juhudi zake zinaonekana kwa kila mtu hadi sasa.

Mbali na hao wapo pia wengine ambao wanaendelea kusumbua kama vile James Maddison ambaye anachezea Leicester City, Felipe Anderson wa West ham, Alisson Becker wa Liverpool, Lucas Digne ambaye msimu uliopita alikuwa Barcelona lakini akatimkia Everton na amekuwa na msimu mzuri sana akiwa kama mchezaji ndani ya klabu hiyo.

3 Komentara

    Ni kweli kabisa.

    Jibu

    Usajil mzur sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.