Kiungo wa klabu ya Arsenal Bukayo Saka ameendelea kuwasha moto akiwa na timu ya taifa ya Uingereza kwenye michuano ya kufuzu michuano ya Euro mwaka 2024 baada ya kufunga bao zuri na kupiga pasi ya bao.
Bukayo Saka alifanikiwa kupiga pasi ya bao la kuongoza kwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa taifa hilo Harry Kane, Kabla ya dakika chache mbele kufunga goli zuri na kuiweka mbele Uingereza kwa mabao mawili kwa bila dhidi ya Ukraine.
Winga huyo ambaye amekua na msimu bora sana akiwa na klabu yake ya Arsenal akiwa mpaka sasa ameshahusika kwenye mabao 22 kwenye ligi kuu ya Uingereza akiwa amefunga mabao 12 huku akiwa amepiga pasi 10 za mabao ikiwa ni wastani mzuri kwa mchezaji huyo.
Saka amekua msaada mkubwa kwa klabu yake ya Arsenal msimu huu kwani kutokana na ubora ambao amekua anauonesha ndani ya msimu huu ni chachu ya mafanikio ya timu hiyo mpaka sasa, Klabu ya Arsenal mpaka sasa inaongoza ligi ya Uingereza mbele ya klabu ya Manchester City kwa alama nane.
Winga Bukayo Saka mbali na kua msaada mkubwa kwa klabu yake ya Arsenal sasa amegeuka na kua moja ya wachezaji mahiri na muhimu ndani ya timu ya taifa ya Uingereza alionesha hilo kwenye michuano ya kombe la dunia, Lakini mpaka sasa kwenye mechi za kufuzu Euro 2024 leo akihusika kwenye magoli yote mawili ya Uingereza kwenye ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya Ukraine.

