Mohamed Salah siku ya jumapili aliingia kwenye kumbukumbu za ligi kuu ya Uingereza kwa kufikisha goli 100 baada ya kufunga katika mechi yao dhidi Leeds United.
Salah ameungana na wachezaji watano ambao waliweza kufunga magoli 100 mapema zaidi katika kumbukumbu za ligi kuu ya Uingereza.

AXA Training Centre iliandaliwa hafla ya wafanyakazi wote na wachezaji kumpongeza na ilitengenezwa jezi maalum yenye namba 100, na wakakusanyika wote kwa picha ya pamoja.
Salah anashika nafasi ya tano katika mtiririko huo huku Alan Shearer akiongoza, pia akishika nafasi ya pili kwa wachezaji wa kiafrika wenye idadi nyingi ya magoli huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Didier Drogba aliyefunga magori 104 akiwa na Chelsea.
| Wachezaji | Tarehe ya kufikisha goli 100 | Idadi ya mechi |
| Alan Shearer | 30/12/1995 | 124 |
|---|---|---|
| Harry Kane | 4/2/2018 | 141 |
| Sergio Aguero | 19/4/2016 | 147 |
| Thierry Henry | 10/2/2004 | 160 |
| Mohamed Salah | 12/9/2021 | 162 |
Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!


