Demba Ba Astaafu Kucheza Soka.

Mashabiki wa Newcastle United, West Ham United na Chelsea wanamkumbuka vizuri mchezaji wao wa zamani, Demba Ba. Ba ameamua kustaafu kucheza soka.

Akiwa na umri wa miaka 36 kwa sasa, Demba Ba amefikia uamuzi wa kustaafu soka ikiwa ni muda mfupi toka ameachana na timu ya FC Lugano ya nchini Switzerland.

Ba anaachana na soka baada ya kuwa mchezaji kwa miaka 16, ametwaa mataji mawili ya Ligi ya Uturuki alipokuwa na Besiktas (2016/17) na mwaka 2019/20 alipokua na timu ya Istanbul Basaksehir.

Sambamba na kucheza soka ngazi ya vilabu, Ba aliitumikia timu ya Taifa ya Senegal katika jumla ya michezo 22. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Demba Ba ameandika;

Kwa moyo uliojaa shukrani, ninatangaza mwisho wangu wa kucheza soka. Imekua ni safari ya aina yake. Licha ya kutokwa jasho na machozi, soka limenipa kumbukumbu na hisia nyingi za kuvutia.


MKWANJA NJE NJE NA DISCO FUNK

Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe