Rais wa klabu ya Lazio inyoshiriki ligi kuu nchini Italia amefunguka kuhusu kiungo nyota klabuni hapo Sergej Milonkovic Savic, Rais huyo amesema kiungo huyo hauzwi klabuni hapo.savicKiungo Saavi amekua akihusishwa kuondoka klabuni hapo kwa muda mrefu sana lakini amekua akiendelea kusalia klabuni hapo. Kiungo huyo ambaye amekua akifanya vizuri katika klabu ya Lazio kwa misimu takribani minne kwasasa.

Kiungo huyo raia wa Serbia ni kiungo bora wa katikati na amekua akihitajika na vilabu kadhaa barani ulaya kama Manchester United,Chelsea pamoja na Barcelona kutokana na ubora mkubwa ambao amekua akiuonesha klabuni hapo.savicRais wa klabu ya Lazio amesisitiza kua kumuuza kiungo huyo fundi ni kitu ambacho hakipo kwenye mipango yake na ana mpango wa kumuongezea mkataba wa muda mrefu Savic klabuni hapo ili aendelee kusalia katika viunga vya Stadio Olimpico.

Hivo ni wazi kua klabu ya Lazio ipo mbioni kumuongezea kandarasi ya muda mrefu kiungo huyo Savic ili aendelee kusalia klabuni hapo ili kuepusha presha wanayoipata Lazio pindi dirisha la usajili linapokua linafunguliwa.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa