Klabu ya Simba SC imeanza vyema michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua ya makundi baada ya kuichakaza ASEC Mimosas mabao 3-1 mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

 

simba sc, Simba SC Yaanza Vizuri Shirikisho Afrika., Meridianbet

Mshambuliaji wa Simba SC, Pape Sakho alifunga bao la kwanza kwa ‘tiktak’ dakika ya 12 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe.

Dakika ya 45, Peter Banda wa Simba SC alipoteza nafasi ya wazi baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mohamed Hussein na kumpiga chenga mlinda mlango wa ASEC kabla ya shuti lake kupaa juu.

Dakika ya 59 ASEC walisawazisha bao kupitia kwa Ki Aziz kwa shuti la mguu wa kushoto baada ya walinzi wa Simba SC kuzembea kuondoa hatari.

Shomari Kapombe aliiandikia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 78 baada ya Yusuf Mhilu kufanyiwa madhambi na mlinda mlango wa ASEC.

Dakika moja baadaye Banda alifunga bao la tatu akimaliza mpira wa krosi uliopigwa na Nahodha John Bocco.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa