Mabingwa wa Tanzania, Simba SC wamefanikiwa kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya FC Platinums ya Zimbabwe leo Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Simba SC inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1 kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumatano iliyopita mjini Harare.

Hii inakuwa mara ya tatu kwa Wekundu hao wa Msimbazi kutinga hatua ya makundi baada ya mwaka 2003 walipoitoa Zamalek ya Misri waliokuwa mabingwa watetezi na 2018 walipoitoa Nkana FC ya Zambia.
Simba SC inayofundishwa na Mbelgiji, Sven Ludwig Vandenbroeck ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Erasto Edward Nyoni kwa penalti dakika ya 39 baada ya beki mwenzake, Shomari Salum Kapombe kuvutwa jezi na Tawana Chikore.

Kipindi cha pili Kapombe akaifungia Simba SC bao la pili dakika ya 61 akimalizia mpira uliotemwa na kipa Francis Tizayi kufuatia shuti la kiungo Mzambia Rally Bwalya.
Nahodha John Raphael Bocco aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya mshambuliaji mwenzake, Mnyarwanda Meddie Kagere akaifungia Simba SC bao la tatu dakika ya 90 na ushei akimalizia pasi ya Bwalya tena.
Mzambia mwingine, Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania, kiungo Clatous Chotta Chama akaifungia Simba SC bao la nne kwa penalti dakika ya 90 na ushei baada yay eye mwenyewe kuvutwa kwenye boksi na Gift Bello.

Kagere aliingia dakika ya 76 kuchukua nafasi ya mshambuliaji mwingine, Mkongo Chris Mutshimba Kope Mugalu lakini akaumia dakika ya 85 na nafasi yake ikachukuliwa Bocco.
Droo ya hatua ya makundi ya michuano hiyo itafanyika Ijumaa Saa 8:00 mchana makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjini Cairo, Misri.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Joash Onyango, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Rally Bwalya, Said Ndemla/Ibrahim Ame dk60, Chris Mugalu/Meddie Kagere dk76/John Bocco dk85, Clatous Chama na Luis Miquissone.
FC Platinums; Francis Tizayi, Gift Mbweti, Nomore Chinyerere, Gift Bello, Ralph Kawondera, Donald Dzvinyai, Kelvin Madzongwe, Rahman Kutsanzira, Khumalo Denzel/Raphael Muduviwa dk58, Perfect Chikwende na Tawana Chikore.
Ndio, kwetu Mteja ni mfalme. Jiunge sasa na familia ya Meridianbet bila malipo yeyote na sisi tutakuzawadia bonasi ya shilingi 3,500 kama sehemu ya kukukaribisha kwenye familia hii BURE!!!. Unasubiri nini??



Samira
Simba mnyama mkali
Lydia Emmanuel Magoti
Safiii Sana akuna Kama simba simba kiboko yao
Shakila mrope
Ongera san wanasimbaa
Adelta
Simba wamejuwa kuwafurahisha mashabiki
Rahmal
Simba baba lao watu jana walijua kufurai
Gabriel
Simba wacheza vzur sana game yako Safi sana
Magdalena
Simba mpira mzuri waliucheza
warda
Simba hii ipo moto sana
Sania
Simba baba lao
Neema juma
Pongezi kwao Simba
Tatu
Hongera simba
Sabrina
Simba Kama Simba
Asia Abdy
Mnyamaaaa
Dorophina
Pongezi kwao simba
Saupha mohamed
Simba babalooo
Angelina
Simba bingwa
Issa
Simba wajitahid
Hopemwaikuka
Simba juu
Sarah
Simba wako vizuri