Ni rasmi sasa vijana wa Gomez wanahitaji alama moja tu ili ifanikiwe kuwa bingwa wa ligi kuu Tanzania bara. Klabu hii yenye maskani yake maeneo ya msimbazi ilirudisha aina yake ya ushindi baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Yanga.
Simba walikuwa ugenini kucheza na KMC katika mechi ya kiporo iliyotakiwa kuchezwa mwezi mei kabla ya wana wa telanga kuelekea kwenye majukumu ya kimataifa.
Katika mechi ya jioni ya leo, Chris Mugalu ndiye aliyekuwa mchezaji bora wa mechi baada ya kutupia bao mbili pekee ambazo zilidumu mpaka dakika tisini baada ya lile moja kukataliwa na kutokana na Offside.
Wanamsimbazi sasa wataelekeza mbio zao za ubingwa kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Coastal Union ambao utachezwa tarehe 11 mwezi huu.
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!


Issa
Tukutane kigoma