Ten Hag: Akubali Kumzungumzia Sancho

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag hatimaye amekubali kutoka taarifa kuhusu mchezaji wake Jadon Sancho baada ya kutokuonekana kwa muda mrefu.

Mchezaji Jadon Sancho kwa kpindi kirefu amekua sio sehemu ya timu ya Manchester United, Na hata mara ya mwisho kuonekana katika mchezo wa klabu hiyo ilikua mwezi wa kumi katika mchezo dhidi ya Chelsea uliomalizka kwa suluhu ya goli moja kwa moja.ten hagJadon Sancho Pia hakuonekana katika kambi ya klabu hiyo iliyowekwa nchini Hispania wakati michuano ya kombe la dunia ikiuendelea nchini Qatar, Na hiyo imepelekea kocha Erik Ten Hag kukumbana na maswali mengi ya waandishi wa habari.

Kocha Ten Hag ameweka wazi kua mchezaji huyo atarejea rasmi ndani ya klabu hiyo katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kati ya klabu hiyo dhidi ya Nottingham Forest tarehe 27 mwezi huu, Hivo kwasasa anaendelea na programu yake maalumu.ten hagMchezaji Sancho kwa kipindi kirefu amekua chini ya kiwango ndani ya klabu hiyo kitu kilichomfanya kukosa nafasi ya kupata nafasi klabuni hapo, Ndipo kocha wa klabu hiyo alipompatia programu maalumu ili kurudisha ubora wake.

Acha ujumbe