Ten Hag Bado Anamfukuzia De Jong

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag inaelezwa bado anaendelea kumfukuzia kiungo wa klabu ya Fc Barcelona raia wa kimataifa wa Uholanzi Frenkie De Jong.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Manchester United zinaeleza kua kocha huyo hajakata tamaa ya kupata saini ya Frenkie de Jong licha ya kumkosa kwenye dirisha kubwa lililopita, Moja ya eneo ambalo Ten Hag anataka kuliimarisha tena ni katikati mwa kiwanja.ten hagFrenkie De Jong ambaye alisalia ndani ya klabu ya Barcelona baada ya Man United kumkosa kwenye dirisha lililopita, Huku kiungo akionesha bado anahitaji kubaki ndani ya Barcelona lakini taarifa zinaeleza kiungo huyo hakutaka kuondoka kwakua alikua anaidai klabu hiyo.

Matumaini ya klabu ya Manchester United ni kua klabu ya Barcelona bado watajaribu kuuza baadhi ya wachezaji wao wawili wanaopokea kiwango kikubwa cha pesa ndani ya timu hiyo kutokana na tatizo la pesa ambalo limekua likiwasumbua klabu hiyo kwa miaka kadhaa sasa.ten hagKocha wa Manchester United Erik Ten Hag anamuona Frenkie De Jong kama mchezaji muhimu sana kwenye falsafa ya mpira wake, Na ndio sababu kubwa ambayo imekua ikifanya kocha huyo kuhitaji huduma ya kiungo huyo hata baada ya kumkosa dirisha lililopita lakini hajakata tamaa na anaamini atamvuta kiungo kwenye viunga vya Old Trafford.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.