Nyumbani Tennis Davis Cup

Davis Cup

tenisi

Tenisi: Mapacha-Bob na Mike Wamestaafu

32
Wachezaji wa tenisi mapacha kutoka Marekani - Bob na Mike Bryan wametangaza kustaafu kucheza mchezo huo wakiwa na umri wa miaka 42 kwa sasa. Mapacha hawa wanatambulika kama moja ya timu bora katika mchezo wa tenisi, wameshinda michezo 119 wakiwa...
tennis

Tennis Yaongoza Orodha ya Matajiri.

20
Utafiti uliofanywa na jarida la Forbes, umeonesha wachezaji wanawake wanaocheza mchezo wa Tennis ni miongoni mwa wanamichezo matajiri duniani. Katika orodha ya wachezaji 10, 9 wanacheza mchezo wa Tennis wakati 1 ni mcheza soka wa timu ya taifa ya Marekani...

Ujue Mchezo wa Tennis na Historia Yake.

45
Tennis (tenisi) ni aina ya mchezo unaochezwa na watu wawili au wanne wakishindana kwa kupiga mpira mdogo kwa raketi kwenye uwanja wa tennis. Shabaha ni kupiga mpira kwa upande wa mpinzani kwa namna inayomshinda kurudisha mpira. Akishindwa kurudisha mpira...

Andy Murray Kushiriki Mashindano ya Tennis ya Kujitolea

38
Mwana michezo wa mchezo wa Tennis Andy Murray amepanga kucheza shindano la kujitolea lililo andaliwa na kaka yake Jamie ambalo litasaidia kuchangia pesa kwenye Idara ya Afya ya Uingereza. Pambano hilo lililopewa jina la linatarajiwa kufanyika bila mashabiki...
Wale mabingwa watetezi wa michuano ya tenisi iliyopewa jina la Davis Cup walianza vibaya kwenye michuano hiyo mwishoni mwa mwaka jana mara baada ya kuchezea kichapo cha 3-0 walipomenyana na timu ya taifa ya Urusi. Kuna tofauti kubwa kati ya michuano mingine ya tenisi na ile ya Davis Cup. Katika michuano ya kuwania kombe la Davis Cup timu hupata ushindi wa idadi ya magoli kama katika mpira wa miguu na ndiyo maana utakuta timu imepigwa 2-1 huku nyingine 3-0. Usishangae. Kisha ushindi huo unapatikana mara baada ya kila timu kuwa na wachezaji wawili katika uwanja kwenye mechi husika. Hatua ya kwanza mchezaji mmoja wa taifa moja anakipiga kwenye mechi na mchezaji wa taifa lingine kisha mchezaji anayeshinda basi timu yake inahesabika kuwa imefunga goli la kwanza kwao. Kinachofuatia ni mtanange wa pili kwa wachezaji wale wawili ambao nao wanakipiga katika mechi moja ambapo anayeshinda maana yake ndiyo anaipa goli timu yake. Mwisho inafuatia mechi ya mchanganyiko ambapo wachezaji wawili wa timu A wanakutana na wachezaji wawili wa timu B husika na mara baada ya mechi hiyo matokeo kamili yanakuwa yameshapatikana tayari. Mchezaji Borna Gojo alipigwa kwa jumla ya seti 6-3 6-3 huku Andery Rublev na Borna Coric naye akipigwa kwa jumla ya seti 6-7 (4-7) 6-4 6-4 alipomenyana na Karen Khachanov na matokeo yakawa ni 2-0. Wachezaji hao waliungana na kuwa wawili kila upande huku Croatia wakifungwa tena na kufanya matokeo yao kuwa 3-0. Katika mtanange wa kundi F, wachezaji wa taifa la Canada, Vasek Pospisil pamoja na Denis Shapovalov wote walichukua ushindi katika mechi zao dhidi ya wachezaji wa taifa la Italia ila walifungwa kwenye mechi ya wawili kwa wawili. Baadaye wakafanikiwa kuibuka na ushindi wa 2-1 katika gemu hiyo. Naye Pospisil alimtandika Fabio Fognini kwa jumla ya seti 7-6 (7-5) 7-5 na Shapovalov akimchabanga Matteo Berrettin kwa jumla ya seti 7-6 (7-5) 6-7 (3-7) 7-6 (7-5) ambapo sasa matokeo ya awali yakawa ni 2-0. Wachezaji hao wa Italia walipojiunga wawili waliwafunga wachezaji wa Canada ambao nao walicheza wawili uwanjani. Michuano hiyo ilikutanisha jumla ya mataifa 18 yaliyoshiriki yakiwa yamepangwa kwenye jumla ya makundi 6. Kundi A: Ufaransa, Serbia, Japan. Kundi B: Croatia, Hispania, Urusi Kundi C: Argentina, Ujerumani, Chile Kundi D: Ubelgiji, Australia, Colombia Kundi E: Uingereza, Kazakhastan, Uholanzi Kundi F: USA, Italia, Canada Mastaa waliokuwemo Kulikuwa na wachezaji mastaa walioshiriki ambao ni pamoja na Rafaael Nadal (Hispania), Novak Djokovic (Serbia), Matteo Berrettin (Italia) ambao wote walitoka katika gemu za ATP na wengine ni akina Roberto Bautista (Hispania), Gael Monfils (Ufaransa), David Goffin (Ubelgiji), Fabio Fognini (Italia), Diego Schwartzman (Argentina), Denis Shapovalov (Canada), Keren Khachanov (Urusi) na Alex de Minaur (Australia).

Tujikumbushe Davis Cup: Mabingwa Watetezi Croatia Walichakazwa!

27
Wale mabingwa watetezi wa michuano ya tenisi iliyopewa jina la Davis Cup walianza vibaya kwenye michuano hiyo mwishoni mwa mwaka jana mara baada ya kuchezea kichapo cha 3-0 walipomenyana  na timu ya taifa ya Urusi. Kuna tofauti kubwa kati ya...
Siku ya Jumapili staa wa kabumbu kutokea klabu ya soka ya Barcelona ya nchini Hispania, Gerard Pique alisema kuwa yeye bado ana matumaini juu ya fainali za michuano ambayo inadhaminiwa na kampuni yake, Davis Cup na kuwa itaendelea katika jiji la Madrid mwaka huu huu. Kundi la wawekezaji la Pique, Kosmos lina dili la miaka 25 yenye thamani ya jumla ya dola bilioni 3 baina yake na International Tennis Federation! Hata hivyo, anaamini kuwa mwezi Novemba kati ya tarehe 23-29 kutakuwa na fainali za kombe hilo nchini Hispania katika mji mkuu wa taifa hilo ingawa kuna balaa la ugonjwa wa Corona kwa sasa. “Mambo hayatabiriki kabisa, tunajaribu kuwa na uelewa wa kitu ambacho serikali itaamua juu ya michezo yote na endapo tutaweza kuwa na mashabiki ama lah ndani ya Caja Magica," alisema hayo Pique wakati akiongea na kituo cha televisheni cha Movistar. "Ninaweza kusema kwamba bado nina matumaini makubwa kwa sababu michuano ya Davis Cup bila ya uwepo wa mashabiki haipendezi kabisa. “Ninafikiri kuwa hakuna mtu ambaye ana uhakika juu ya yatakayokuja kutokea siku za mbeleni na juu ya kuingia uwanjani tukiwa na mashabiki ama bila ya wao kuwepo. Kadri ambavyo siku zinakwenda mbele ndivyo tunaona ni kwa namna gani tutatambua hali itakavyokuwa kiuhalisia zaidi.” Hispania, moja ya taifa ambalo limeathiriwa sana na ugonjwa huu, limekuwa na majadiliano juu ya namna ya kulegeza baadhi ya masharti ya kukaa ndani wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa ambao ulianza kushika hatamu tangu katikati ya mwezi wa tatu mwaka huu. Kuna mipango kuwa wanaotakiwa kuhudhuria endapo kutakuwa na jukwaa la wazi ni watu wapatao 400 pekee na watu 50 endapo watakuwa ndani ya uwanja. Hispania ilishinda tuzo ya Davis Cup mwaka 2019, walipowapiga Canada 2-0 katika fainali iliyofanyika kule kule mjini Madrid ikiwa ni toleo la kwanza la michuano hiyo iliyoboreshwa zaidi. Tangu mwezi wa tatu tarehe za katikati kumekuwa na zuio la uendeshaji wa michuano ya tenisi duniani ambapo pia Wimbledon ilifutwa kwa mara ya kwanza kabisa tangu vita vya pili vya dunia viishe na Roland Garros ikahamia mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu. Inatarajiwa kuwa ATP na WTA itarejea tena ifikapo JUlai 13 mwaka huu endapo mambo yakiwa sawa kiafya.

Gerard Pique Ana Matumaini na Fainali za Davis Cup

20
Siku ya Jumapili staa wa kabumbu kutokea klabu ya soka ya Barcelona ya nchini Hispania, Gerard Pique alisema kuwa yeye bado ana matumaini juu ya fainali za michuano ambayo inadhaminiwa na kampuni yake, Davis Cup na kuwa itaendelea katika...
Osaka Alamba Ulaji na Nike

Osaka Alamba Ulaji na Nike

2
Mara nyingi wadhamini huwa na mchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya mchezaji hasa katika kujenga wasifu wake. Jambo hilo mara nyingi huwafanya wachezaji wengi kuhangaika nalo ili angalau waweze kuwa na wale ambao watawapa changamoto na ramani za wao...

Ubabe wa Federer na Nadal

2
  Nyota wa tenisi, Roger Federer amekumbushia historia yake ya maisha ya tenisi kwa miaka 15 iliyopita siku alipokutana kwa mara ya kwanza uwanjani na Rafael Nadal na alipopoteza mechi hiyo kutoka kwa mpinzani wake. Jambo hilo linamkumbusha mbali sana...

MOST COMMENTED

Ukikohoa Makusudi Kadi Nyekundu!

41
Janga la Corona limeendelea kutufanya tukishuhudia mabadiliko megi katika taratibu, sheria na uendeshaji wa michezo ulimwenguni, soka halijatupwa katika mabadiliko haya. Unaweza kupata kadi...
Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

HOT NEWS