Liverpool na Rangers wapo kundi moja Ligi ya Mabingwa ya Uingereza hatua ya makundi; Erling Haaland kuwakabiri tena waajiri wake wa zamani Borussia Dortmund; Chelsea kukutana na Milan, Salzburg na Zagreb katika Kundi E; Spurs kumenyana na Frankfurt, Sporting, Marseille; Celtic watakuwa na  mabingwa wa UCL Real Madrid katika Kundi F

Liverpool na Rangers zitamenyana katika kundi moja kwenye Ligi ya Mabingwa baada ya kupangwa Kundi A. Timu hiyo ya Scotland, ambayo iliishinda PSV siku ya Jumatano na kufuzu hatua ya makundi, itamenyana na Wekundu hao kwa mara ya kwanza katika mechi ya mashindano, pamoja na michezo ya makundi dhidi ya mabingwa wa Uholanzi Ajax na Napoli ya Italia.


Erling Haaland ataungana na Manchester City kuikabri klabu yake ya zamani ya Borussia Dortmund baada ya Manchester City, waliofuzu nusu fainali msimu uliopita, kupangwa pamoja na Sevilla, FC Copenhagen katika Kundi G.

Chelsea itamenyana na mlinzi wao wa zamani Fikayo Tomori baada ya washindi wa mwaka 2021 kuunganishwa na AC Milan katika Kundi E. Vijana wa Thomas Tuchel pia watamenyana na Salzburg na Dinamo Zagreb na wanapewa nafasi kubwa ya kutinga hatua ya mtoano.

Tottenham, waliofika fainali mwaka wa 2019 na wamerejea kwenye kinyang’anyiro hicho kwa mara ya kwanza tangu 2020, wapo kwenye kundi moja pamoja na washindi wa Ligi ya Europa, Eintracht Frankfurt, Sporting Lisbon na Marseille katika Kundi D.

Mabingwa wa Scottland Celtic watachuana na mabingwa watetezi wa UEFA , Real Madrid katika mchezo mzuri wa Kundi F, pamoja na mechi dhidi ya RB Leipzig na Shakhtar Donetsk huku wakirejea hatua ya makundi kwa mara ya kwanza tangu 2017.

Droo kamili ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa (UCL) Iko hivi.

Kundi A: Ajax, Liverpool, Napoli, Rangers.
Kundi B: Porto, Atletico Madrid, Bayer Leverkusen, Club Brugge.
Kundi C: Bayern Munich, Barcelona, ​​Inter Milan, V Plzen.
Kundi D: Frankfurt, Tottenham, Sporting, Marseille.
Kundi E: AC Milan, Chelsea, Salzburg, Dinamo Zagreb.
Kundi F: Real Madrid, Leipzig, Shakhtar Donetsk, Celtic.
Kundi G: Man City, Sevilla, Borussia Dortmund, Copenhagen.
Kundi H: PSG, Juventus, Benfica, Maccabi Haifa.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa