Utafiti uliofanywa na jarida la Forbes, umeonesha wachezaji wanawake wanaocheza mchezo wa Tennis ni miongoni mwa wanamichezo matajiri duniani.

Katika orodha ya wachezaji 10, 9 wanacheza mchezo wa Tennis wakati 1 ni mcheza soka wa timu ya taifa ya Marekani – Alex Morgan.

Wafahamu wacheza Tennis matajiri duniani.
  1. Naomi Osaka
tennis
Naomi Osaka

Osaka anauraia wa nchi mbili lakini aliamua kuichagua kuipeperusha bendera ya Japan kwenye Michuano ya Tokyo 2020 Summer Olympic. Anamapato ya dola za kimarekani milioni 37.4. Uamuzi wake umepatia faida kubwa kibiashara ambapo anafanyakazi na makampuni yanayodhamini Michuano ya Olympic kama vile Procter & Gamble, All Nippon Airways and Nissin. Ni Roger Federer pekee anatengeneza pesa ndefu kupitia matangazo kumzidi Osaka.

 

2. Serena Williams

tennis
Serena Williams

Anamapato ya dola za kimarekani milioni 36. Kupitia ushirikiano wa kibiashara na makampuni kama Nike, Gatorade, Procter & Gamble,  na Beats, kunamuongezea Serena wigo wa mashabiki na kufikia milioni 40 katika mitandao yote ya kijamii – Twitter, Instagram na FaceBook. Serena na mumewe [Alexis Ohanian], ni sehemu ya kikundi cha uwekezaji kilichozawadiwa timu ya National Women’s Soccer League jijini Los Angeles- Marekani. Mtoto wake – Olympia ni sehemu ya kikundi hicho na katika umri wa miaka 2 pekee, anatambulika kama mmliki mdogo wa timu ya michezo.

 

3. Ashleigh Barty.

tennis
Ashleigh Barty

Barty anamapato ya dola za kimarekani milioni 13.1. Alishinda taji lake la kwanza katika Michuano ya French Open mwaka 2019 na kuchagiza kupata bonasi kutoka kwa wadhamini wa michuano hiyo – Fila and Head. Anamikataba ya kibiashara na makampuni kama Rado, Jaguar, Vegemite, Banana Boat na Esmi. Juni 2019, aliweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kutoka Australia kushika nafasi ya 1 toka mwaka 1976.

 

4. Simona Halep

tennis
Simona Halep

Akiwa na mapato ya dola za kimarekani milioni 10.9. Halep alibeba tuzo yake ya pili ya Slam mwaka jana katika Mashindano ya Wimbledon. Anafanyakazi na wafadhili kama Nike, Wilson, Hubolt na Avon.

 

5. Bianca Andreescu

tennis
Bianca Andreescu

Anamapato ya dola za kimarekani milioni 8.9. Aliweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Canada kuwahi kushinda tuzo ya Grand Slam katika Mashindano ya US Open mwaka 2019. Ushindi huo pamoja na uzoefu wake kwa miaka 5, ulimpatia fursa ya kufanya kazi na makampuni kama Nike, Rolex, Gatorade, Royale na Sleep Country.

Katika orodha ya wachezaji wanawake 10 matajiri duniani. Wa 6 ni Garbine Muguruza (dola milioni 6.6), wa 7 ni Elina Svitolina (dola milioni 6.4), wa 8 ni Sofia Kenin (dola milioni 5.8), wa 9 ni Angelique Kerber (dola milioni 5.3) na wa 10 ni Alex Morgan (dola milioni 4.6) ambaye ni mcheza soka.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma zaidi Ucheze

20 MAONI

  1. kiukwel wenzetu wanathamin sana michezo sana na pia wanaonyesha ushabk kwa kila aina michezo ambayo wanayoianzisha hiyo hufanya ushindan wenye faida sana ukiangalia

  2. kiukwel wenzetu wanathamin sana michezo sana na pia wanaonyesha ushabk kwa kila aina michezo ambayo wanayoianzisha hiyo hufanya ushindan wenye faida sana ukiangalia

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa