Wachezaji wa tenisi mapacha kutoka Marekani – Bob na Mike Bryan wametangaza kustaafu kucheza mchezo huo wakiwa na umri wa miaka 42 kwa sasa.
Mapacha hawa wanatambulika kama moja ya timu bora katika mchezo wa tenisi, wameshinda michezo 119 wakiwa na makombe 16 ya Grand Slam.
Mapacha Wamestaafu kucheza Tenisi.
Bob na Mike walitangaza kustaafu baada ya Mashindano ya US Open lakini wamebadilisha maamuzi yao na kuamua kustaafu mapema kabla ya mashindano hayo ambayo yatachezwa bila mashabiki.
“Mashabiki ndio wanaoyafanya Mashindano ya US Open kuwa ya kipekee akili mwetu. Ndio ulikuwa wakati wetu wa kuwaaga mashabiki wetu na kuufurahia uwepo wao kwa mara ya mwisho.” amesema Bob Bryan.
“Kwa umri huu, tunahitaji nguvu kubwa sana kwa ajili ya kushindana, bado tunapenda kucheza lakini hatupendi kuiandaa miili yetu kwa ajili hiyo.” amesema Mike Bryan.
Mapacha hawa walicheza mchezo wao wa kwanza kwa ngazi ya mashindano mwaka 1995. Mwaka 2007 waliisaidia Marekani kushinda kombe la Davis Cup na kushinda medali ya shaba kwenye Mashindano ya Beijing 2008.
Mwaka 2012 na 2013 mapacha hawa walikuwa kwenye ubora mkubwa na kufanikiwa kutwaa makombe yote manne na medali ya dhahabu kwenye Mashindano ya London Olympic.
Beti Mbio za Mbwa Mubashara
Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.


Dorophina
Sio mbaya kwakuwa umri umeshaenda Ni muda wao wa kustaafu
Khadija
duh miaka 42 kweli kazi na umri
Sauda
Wakapumzike kwa kweli
Mwajumah
Ni Jambo zuri kupumzisha mwili Kwan umri ushawatupa mkono
Caroline
Umri wao unaruhusu kustaafu.
Ester jackson
Pongezi sana kwa kustaafu pia kustaafu kwenu pakawe chachu ya kunyanyua vipaji kwa vijana
Lydia Emmanuel Magoti
Pongezi Sana kwao mriwao unastairi kustafu hao walio nyuma yenu inabidi wafate nyao zenu ilikunyanyua makombe zaidi nazaidi
rama
kila la kheri mapacha
Shan
Nice
Nasra
Gud news
aisha
Wanasitahili tunzo pia tunawapongeza kwa kazi walioifanya
Mwanahamisi
Pongezi sana kwa kustafu
Furahav
Hongera sana.
Zeiyana
Bob na Mike wana histor kubwa kwenye michezo ya tenis
Sabrina
Nawatakia kila la kheri katika ustaafu wao
farida ahmadi
Kila la kheri
Theonestina
Mapumziko mema kwao
jullie
watumie hela sasa
David Pere
Wanasitahili tunzo pia tunawapongeza kwa kazi walioifanya
Janeflora malisa
Good
magdalena
wapumzike sasa umri ushawatupa mkono
warda
Hongera yao ma best zangu
felister
miaka 42 walikua wana haki ya kustaafu
Tatu
Muda wao umefika kustaafu na umri wao unaluhusu
Shafii
Siku zote kunamaisha mengine baada ya michezo au kitu unachokifanya pongezi kwao.
Antony Luseno
Sio mbaya mchango wao kwenye tennis umeonekana
Rose kapinga
Kazi nzuri wamefanya
neema hassan
Umri umewatupa mkono
Asia Abdy
Safii
Samiah
Wamefanya kazi nzuri
Samira
Wamestahili kustaafu umri umewatupa mkono na tunawashukuru kwa kutuburudisha
[email protected]
Miaka 42 sio mchezo