Tetesi zinasema Arsenal ni miongoni mwa klabu kadhaa zinazoangalia uwezekano wa kumsajili mchezaji wa safu ya ulinzi wa timu ya RB Leipzig Mfaransa Ibrahima Konate mweye umri wa miaka 21.

Konate ni mmoja kati ya wachezaji sita ambao Gunners wanashugulika kuwapata, huku klabu hiyo pia ikiwa tayari kumuuza mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette, 29, kwa bei inayofaa.

Tetesi zinasema kiungo wa kati wa Manchester United, Bruno Fernandes, 26, yuko tayari kusaini mkataba mpya ambao utaongeza mshahara wake mara dufu na kuweza kupata malipo ya takriban pauni 200,000 kwa wiki.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema mlinzi wa Misri Ahmed Elmohamady, 33, ataondoka Aston Villa kwa mkataba usio na malipo msimu huu huku klabu hiyo ikiwa haina mipango ya kumpatia mkataba mpya.

Napoli wamepunguza kiwango cha pesa walizokuwa wanataka kwa ajili ya kumuuza Kalidou Koulibaly hadi kufikia kiwango cha euro milioni 45 (£38.7m) huku Bayern Munich wakiaminiwa kuongoza.

Leicester City wamefufua nia yao kwa mchezaji ambaye wamekuwa wakimtaka kwa muda mrefu Ismail Jakobs, mwenye umri wa miaka 21, lakini the Foxes wanakabiliwa na ushindani kutoka Brighton ambao pia wanamfuatilia kwa karibu mchezaji huyo wa kimataifa kutoka klabu ya Ujerumani ya Cologne.

Manchester United wanatafuta klabu mbadala kwa ajili ya kiungo wa kati Andreas Pereira, 25, msimu huu kwasababu Lazio wanataka kubadilisha makataba wa Mbrazili huo kutoka mkataba wa mkopo na kusaini mkataba wa kudumu.

Tetesi zinasema shinikizo la kifedha linaweza kuilazimisha klabu ya Valencia kumuuza mshambuliaji wa Ureno Goncalo Guedes, 24, ambaye analengwa na West Ham katika msimu ujao.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema Juventus wamemtaja kiungo wa Chelsea Jorginho, 29, kama chaguo lao la pili iwapo watashindwa kusaini mkataba na Muitalia Manuel Locatelli, 23, kutoka klabu ya Sassuolo.

Leeds United wanakabiliwa na ushindani kutoka AC Milan katika kujaribu kusaini mkataba na winga wa Real Madrid na Uhispania Lucas Vazquez, 29, ambaye mkataba wake katika klabu ya Bernabeu unamalizika msimu ujao.

Eintracht Frankfurt wamesema kuwa hawatamzuia mkurugenzi wao wa mchezo Fredi Bobic, 49,kama atachagua kuondoka, huku Manchester United, West Ham na Hertha Berlin wakihusishwa na taarifa za kumnunua Mjerumani huyo.


Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx

Hauihitaji kufikira mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

  CHEZA HAPA

8 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa