Klabu ya soka ya Coastal Union kutokea Tanga, leo imetamatisha mwendo wa michezo 21, bila kufungwa wa vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara klabu ya soka ya Yanga baada ya kuibuika na ushindi wa mabao 2-1.
Coastal imeibuka na ushindi huo katika mchezo mkali uliopigwa kwenye dimba la Mkwakwani jijini Tanga.
Kabla ya mchezo wa leo Yanga ilikuwa imecheza michezo 21 ya Ligi Kuu Bara, bila kupoteza mchezo wowote wakishinda michezo 14 na kutoa sare michezo saba.
Baada ya mchezo Kocha Coastal Union Juma Mgunda amesema kuwa hawakuwa na namna ya kufanya ila mpango wa Mungu ulitimia.
“Hakukuwa na namna ya kufanya kwani vijana wangu niliwaambia kwamba mchezo utakuwa mgumu wanapaswa wapambane ndani ya uwanja.
“Mungu amejibu maombi yetu nasi tumeshinda hivyo ni fuaraha kwetu na mashabiki wetu, mapambano bado yanaendelea,” amesema.
Licha ya kipigo hicho Yanga bado inasalia katika uongozi wa ligi na pointi zao 49, baada ya kucheza michezo 22.
Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx
Hauihitaji kufikira mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.
Bado Yanga ina nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa msimu huu
Hongera yao
Wamewakomesha
Vizur
Safi sana
Safi sanaaa
Vizuri sana
Walinikosha sana