Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema Everton na Leeds United zinamuwania beki wa kushoto wa Real Madrid, Marcelo, Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 33, ambaye hayuko kwenye mipango ya kocha wa Madrid, Carlo Ancelotti.

Tetesi zinasema, Leicester City inungana na vilabu vya Liverpool, Chelsea na Tottenham katika mbio za kumsajili mshambuliaji raia wa Zambia, anayecheze RB Salzburg, Patson Daka (22).

Tottenham inapigana vikumbo na klabu ya Fiorentina kumuwania mshambuliaji wa Stuttgart, Nico Gonzalez, (23), tayari klabu hiyo ya Fiorentina ya Seria A, imeshatenga dau la £21.5m.

Kocha mpya wa Celtic, Ange Postecoglou anamuwania kipa wa Brighton, Mat Ryan, ambaye aliwahi kumfundisha akiwa na timu ya taifa ya Australia.

 

Manchester united

Manchester United inashughulikia uhamisho wa kiungo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 21, Jadon Sancho ikiwemo marupurupu, baada ya klabu yake ya Borussia Dortmund kukataa ofa ya kwanza kutoka Man Utd. Klabu hiyo ya Ligi ya Bundasliga inataka kitita cha £86m kumuachia nyota huyo.

Tetesi zinasema, Arsenal imewasiliana na Manchester United kuhusu uhamisho wa kiungo wa Kidachi mwenye umri wa miaka 24, Donny van de Beek.

Atletico Madrid imeiambia Manchester United kwamba Kieran Trippier ana thamani ya £30mil. Bosi wa Utd, Ole Gunnar Solskjaer anamtaka beki huyo (30), mlinzi huyo wa kulia wa England ili kumpa changamoto ya ushindani, Aaron Wan Bissaka.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amemuweka sokoni mshambuliaji mfaransa, Anthony Martial, 25, kwa sababu ya utukutu, huku Klabu ya Real Madrid ikihusishwa kumsaka.

 

martial
Martial akiteta na Kocha wake Ole Gunnar Solskjaer

Tetesi zinasema, Barcelona itamfahamisha winga wa Ufaransa, Ousmane Dembele (24), kuchagua mawili kusaini mkataba mpya au kuondoka klabuni hapo.

Kocha mpya wa Wolves’ Bruno Lage amefahamishwa kwamba kiungo wa kireno, Ruben Neves, 24, na mshambuliaji wa Kihispania, Adama Traore (25) wako sokoni ili kupata fedha za kuboresha kikosi hicho.

Barcelona inajiandaa kupeleka ofa kwa kiungo wa kihispania, Ilaix Moriba (18), baada ya kuhusishwa na usajili wake hapo awali, lakini pia anafuatiliwa na vilabu vya Manchester City, Chelsea na Manchester United.

Tetesi zinasema, Everton inamtaka mlinda mlango wa Kibrazili, Neto (31) kutoka Barcelona.

Tetesi zinasema, Leeds United imefanya mazungumzo ya awali na Club Bruges kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji wa kidachi, Noa Lang (21).

Mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappe, 22, ameleta sintofahamu mpya kuhusu hatma yake katika klabu ya Paris St-Germain, baada ya kukiri kuwa hajui kama klabu hiyo ni mahala sahihi kwake.

 

Pochettino: Mbappe Asilaumiwe Kwa Kupoteza Gemu

Leeds United inajaribu kuipiku Norwich City katika mpango wake wa kumsajili mlinda mlango wa Southampton, Angus Gunn, baaada ya ada ya uhamisho wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 kufikiwa muafaka.

Mahasimu Bristol City, Cardiff City na Swansea City wameonyesha nia ya kumsajili kiungo aliye huru, Matty James, 29, ambaye anaondoka Leicester City msimu huu, baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka tisa.

Tetesi zinasema, Barcelona wana uhakika wa kukamilisha mpango wa kumsajili mshambuliaji wa kidachi, Memphis Depay (27), ambaye mkataba wake na Lyon, unamalizika wiki ijayo.

Barca pia inajiandaa kumsajili mshambuliaji wa Argentina, Lautaro Martinez (23), baada ya kusitisha mazungumzo yake ya mkataba mpya na klabu yake ya Inter Milan.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

3 Komentara

    Ziko poa

    Jibu

    Asante kwa makala

    Jibu

    Habar nzur

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.