Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Manchester United inampango wa kumfanya kiungo wa Ufaransa Paul Pogba, 28, kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa katika Ligi Kuu ya Uingereza katika mkataba wake mpya wa kima cha paundi milioni 104.

Tetesi zinasema, Borussia Dortmund imeipatia Manchester bei ya mwisho ya paundi milioni 77 na marupu rupu mengine kumsaini winga wa England Jadon Sancho, 21.

Tetesi zinasema, Paris St-Germain wamewasiliana na Real Madrid kuhusu uwezekano wa kumsajili mlinzi wa Ufaransa Raphael Varane, 28.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Arsenal wameanza mazungumzo na Eintracht Frankfurt kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Ureno Andre Silva, 25, ambaye anauzwa kwa karibu £34m msimu huu wa joto.

Tetesi zinasema Chelsea wako tayari kumpatia mkataba mpya wenye donge nono kiungo wa kati wa Ufaransa N’Golo Kante, 30.

Lazio wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Argentina Joaquin Correa,26, ambaye ananyatiwa na Arsenal na Tottenham. Kuna uwezekano Gunners wakamtumia kiungo wa kati wa Lucas Torreira, 25, kama sehemu ya mkataba.

Kiungo wa kati wa Uturuki aliye na umri wa miaka 27- Hakan Calhanoglu, ambaye mkataba wake AC Milan unakamalizika msimu huu, amepewa muda wa mwisho kuamua hatma yake ya baadae licha ya tetesi kwamba Arsenal wanamtaka.

Eintracht Frankfurt wanamtaka winga wa Roma na Uturuki Cengiz Under, 23, ambaye msimu uliopita alikuwa Leicester City kw ammkopo na huenda akauzwa kwaeuro milioni 10 (£8.6m).

 

Tetesi zinasema, West Brom wameonesha ishara ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Stoke City Muingereza Sam Clucas, 30.

West Brom pia wanatarajiwa kumteua mkufunzi wa Barnsley Valerien Ismael kama meneja wao mpya baada ya kufikia kanuni ya makubaliano na Mfaransa huyo aliye na umri wa miaka 45.

Newcastle inatafakari uwezekano wa kuipatia Arsenal ofa ya mchezaji na pesa juu yake katika mkataba ambao utamwezesha kiungo wa kati Muingereza Joe Willock, 21, kurejea nyumbani baada ya kukamilisha mkataba wake wa mkopo msimu uliopita.

 


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao.
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe