Qatar Yatoa Tamko Kuelekea World Cup 2022

Baada ya kupata ukosoaji mkubwa pamoja na watu wengi walionekana kupinga Kombe la Dunia kufanyika kule Qatar, hatimaye nchi hiyo imetoa taarifa rasmi kuhusu mashabiki au wadau wa soka watakaoruhusiwa kuingia kwa ajili ya World Cup 2022.

Qatar ilipewa uenyeji wa mashindano hayo makubwa lakini walipata vipingamizi kwa timu nyingi na hata wadau wa soka. Serikali ya nchi hiyo ilieleza kuwa ilitegemea kufanya mashindano hayo bila uwepo wa Korona lakini janga hilo linalazimika kupatiwa utatuzi.

Waziri mkuu wa nchi hiyo, Sheikh Khalid bin Khalifa amedai kuwa kama serikali wapo katika mazungumzo ya kununua dozi milioni moja ya chanjo ya Corona kwa ajili ya kuchanja wale watakaoingia nchini humo kwa ajili ya World Cup 2022.

Nchi hiyo itafanya majaribio ya kuona idadi ya watu watakaoweza kuingia katika michuano hiyo mikubwa kwa kutazama maendeleo ya michuano ya 2021 Arab Cup baadae mwaka huu.

Qatar imefanikisha kutoa chanjo takribani 50.8% kwa wananchi wake na wanaendelea kutoa dozi hizo ili kuhakikisha kuwa nchi hiyo inakuwa huru kabisa kutokana na janga hilo la Corona huku ikiruhusu watu wakifurahia soka katika World Cup 2022.

USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe