Tetesi zinasema, Manchester City huenda ikatangaza usajili wake ghali wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Mnorway Erling Braut Haaland, 2 wiki inayokuja.

Liverpool inaongoza mbio zinazozijumuisha pia klabu za Real Madrid na Chelsea katika kuwania saini ya kiungo mfaransa na Monaco, Aurelien Tchouameni, 22.

Arsenal inaweza kugonga mwamba katika mpango wake wa kumsajili mshambuliaji Muargentina Lautaro Martinez, 24 ambapo Inter Milan inaonekana haitamuuza.

Barcelona Warejesha Nia Yao na Lautaro Martinez

Tetesi zinasema, Arsenal, Chelsea na Manchester United zinamuwania kiungo wa RB Leipzig mfaransa Christopher Nkunku, 24, msimu huu.

Tetesi zinasema, Bayern Munich inaandaa ofa ya kwanza ya £15m ili kuanza mazungumzo na RB Leipzig kwa ajili ya kiungo wake muaustria Konrad Laimer.

Kiungo wa zamani wa Manchester United David Beckham ana matumaini mshambuliaji mreno Cristiano Ronaldo, 37, atasalia Old Trafford msimu ujao.

 

Cristiano Ronaldo

Kiungo wa zamani wa Uholanzi Fred Rutten amefichua kwamba amekataa ofa ya kuwa mmoja wa wasaidizi wa Erik ten Hag, Manchester United akijiandaa kurudi PSV Eindhoven.

Tetesi zinasema, Liverpool wanamatumaini ya kuipiku Leeds katika usajili wa £4m wa mlinzi wa Aberdeen na Scotland Calvin Ramsay,19. Kinda huyo anaandaliwa kumsaidia Trent Alexander-Arnold.

Meneja wa zamani wa Chelsea na Spurs Andre Villas-Boas anaweza kuwa kocha wa Morocco, na kufungua milango ya kurejea kwa Hakim Ziyech kwenye timu ya taifa.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa