Tetesi zinasema, Manchester United itaingia katika mbio za kumsaka mshambuliaji wa Poland, Robert Lewandowski iwapo ndoto za mkongwe huyo mwenye miaka 33 kujiunga na Barcelona zitashindwa kutimia.

Liverpool imefikia makubaliano ya kumnunua mshambuliaji wa Uruguay, Darwin Nunez, 22 kutoka Benfica na sasa wanaanda mkataba tu kukamilisha uhamisho huo wenye thamani ya £85m.

Tetesi zinasema, Tottenham wako kwenye mazungumzo mazuri ya kumsajili mshambuliaji wa Everton na Brazil Richarlison, 25, kwa ada ya £51m.

 

Richarlison to Real Madrid

Chelsea wamepata imani kubwa ya kumsajili winga mfaransa, Ousmane Dembele baada ya klabu yake ya Barcelona kuthibitisha kwamba Dembele, 25, hajasaini mkataba mpya.

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Christopher Nkunku, 24, anatarajia kubaki RB Leipzig na kusaini mkataba mpya licha ya kuwaniwa na Manchester United na Chelsea.

Arsenal ni moja ya klabu kadhaa zinazofuatilia kinachoendelea kwa Marco Asensio pale Real Madrid, hatma ya kiungo huyo mshambuliaji wa Hispania mwenye miaka 26 itajulikana wiki ijayo.

Tetesi zinasema, Kiungo mfaransa Paul Pogba, 29, atarejea Juventus kwa mkataba wa miaka minne wenye thamani ya £68m baada ya kuachana na Manchester United.

Fulham wana matumaini ya kuwasajili na nyota wawili wa Liverpool, mlinzi wa pembeni raia wa Wales, Neco Williams, 21 na mshambuliaji mjapani Takumi Minamino, 27.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Kiungo wa Switzerland Granit Xhaka, 29, anasakwa na Bayer Leverkusen wakati huu ambapo Arsenal anakaribia kumnasa kiungo mchezeshaji wa Ubelgiji Youri Tielemans, 25, kutoka Leicester.

Tetesi zinasema, Luis Suarez bado hajaamua hatma yake lakini Aston Villa inataka kumsajili mshambuliaji huyo mruguay mwenye miaka 35.

Juventus iko kwenye mazungumzo na Atletico Madrid kumsajili kwa mkataba wa kudumu mshambuliaji wa zamani wa Chelsea mhispania, Alvaro Morata, 29.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa