Tetesi zinasema, Kiungo wa kati wa Leeds United na England Kalvin Phillips, 26, ameiambia klabu hiyo anataka kuondoka msimu huu ili kujiunga na Manchester City.

Wawakilishi wa kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United Paul Pogba wanakaribia kukamilisha mkataba wa miaka minne kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, 29, kujiunga na Juventus kwa uhamisho wa bure.

Chelsea wameanza mazungumzo juu ya kurejea kwa mkopo Romelu Lukaku kwenda Inter Milan, lakini mshambuliaji huyo wa Ubelgiji, 29, atalazimika kukatwa mshahara.

 

Chelsea

Everton wamekamilisha usajili wa beki wa Uingereza James Tarkowski, 29, kwa uhamisho huru kutoka Burnley lakini mpango huo hautarajiwi kutangazwa hadi mwisho wa Juni.

Tetesi zinasema, Manchester United wanapigiwa upatu kumsajili kiungo wa kati wa Porto na Ureno Vitinha, 24, ambaye ana kipengele cha kuuzwa chenye thamani ya £34m.

Matumaini ya Chelsea kumsajili mlinzi wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde hayatakwama licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kufanyiwa upasuaji wiki hii.

Arsenal bado wanaweza kumsajili kiungo wa kati wa Hispania Marco Asensio, 26, msimu huu huku mzozo kuhusu mshahara wake Real Madrid ukiendelea.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Real Madrid wanatumai kumsajili kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Uingereza Jude Bellingham, 18, licha ya ushindani kutoka kwa timu za Ligi kuu England za Manchester United na Liverpool kuhusu mkataba wa £78m.

Tetesi zinasema, Southampton wamefikia makubaliano na Manchester City kumsajili kipa wa Ireland Gavin Bazunu, 20.

Bournemouth wanakaribia kumsajili beki wa West Ham Muingereza Ryan Fredericks, lakini Fulham pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa