Klabu ya Tottenham leo itashuka dimbani katika mchezo wa kombe la Fa raundi ya tatu dhidi ya vijana wa Vicent Kompany klabu ya Burnley ambapo Spurs watakua katika dimba lao la nyumbani.
Tottenham imebaki kwenye michuano miwili tu msimu huu ikiwemo kombe la Fa hivo mchezo wa leo dhidi ya Burnley utakua moja ya michezo muhimu kwa klabu hiyo chini ya kocha Ange Postecoglou.Vijana hao wa kocha Ange tayari walishatupwa nje kwenye michuano ya Carabao hivo kwasasa wanashiriki michuano miwili pekee ya ndani ambayo ni ligi kuu na Fa, Huku ligi kuu ikionekana ni mlima mrefu kwa upande wa Fa inaonekana kama mlima sio mkubwa sana.
Tottenham wana muda mrefu hawajatwaa taji lolote hivo msimu huu inaweza kua nafasi ya wao kutoa gundu la muda mrefu la kukosa taji, Kupitia mchezo wa leo dhidi ya Burnley safari yao ya matumaini inaweza kuanza rasmi.Klabu ya Burnley nayo imekua kwenye kiwango kizuri hivi karibuni hivo mchezo unatarajiwa kua mgumu na sio wa upande mmoja, Mchezo utakua wa ushindani kwa pande zote ambapo Spurs wao watakua wanapambana kuanza safari ya kulitafuta taji lao la kwanza baada ya muda mrefu.