Bondia Tyson Fury amempiga kwa mara nyingine Deontay Wilder kwa KO round ya 11 na kufanikiwa kutetea ubingwa wake wa WBC kwenye pambano liliopigwa leo T Mobile Arena, Nevada, Marekani.

Baada ya miezi 12 tangu Fury,32 achukue ubingwa huo kutoka katika mikono ya Wilder, ameendeleza ubabe baada ya kumpiga katika mapambano mawili yaliopita katika raundi ya 4.
Wilder alipambana mpaka raundi ya 10 akionyesha ubora wake kabla ya kudondoshwa katika raundi ya 10, kabla ya refa kupuliza filimbi katika raundi ya 11 baada ya kudondoshwa chini kwa mara nyingine.
“Nilidondoka mara kadhaa, Niliumia, Wilder ni bondia mgumu/bora,” alisema Fury.
“Ni pambano zuri sana, Sina sababu yoyote, Wilder ni bondia bora, amenifanya nipiganie pesa zangu. Siku zote nasema mimi ni bondia bora duniani na yeye ni wa pili.
“Usijaribu kunishuku. Wakati karata zote ziko chini mimi ndo nafanikisha.” aliongeza.
SPACE SPIN NA MERIDIANBET.
Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.


