UEFA Kulegeza Masharti Kuendana Na COVID-19

Ni dhahiri, misimu miwili [na huu ni msimu wa 3] iliyopita, imeathiriwa sana na COVID-19. UEFA imeweka milango wazi ili kuendana na hali halisi.

Kumekuwa na makubaliano ya kimkataba kati ya UEFA na mashirikisho ya soka barani ulaya kuhusu kupangwa kwa michezo ya ligi na makombe ya ndani siku ambazo kuna michezo ya Ligi ya Mabingwa.

Haya ni makubaliano ya kimkataba ambayo, michezo ya ligi na makombe ya ndani, haipaswi kuchezwa usiku mmoja na michezo ya Ligi ya Mabingwa. Lakini, kutokana na madhara makubwa yanayotokana na maambukizi ya COVID-19, hili linaweza kulegezwa kwa kiasi.

Kwa EPL pekee, tayari michezo 18 imeshaghairishwa kwa msimu huu pekee, hii inapelekea kuwa na idadi kubwa ya michezo ambayo haichachezwa wakati msimu ukiwa unaelekea kwenye hatua za mwishoni. Ili kupunguza msongamano wa michezo, Uefa wameruhusu baadhi ya michezo kuchezwa kwenye siku zilizopangwa kwa Ligi ya Mabingwa.

Japokuwa, michezo hiyo itaruhusiwa endapo hakutakuwa na namna nyingine yeyote ya michezo hiyo kuchezeka na hivyo, makubaliano yatafanyika kwa kuzingatia mchezo mmoja mmoja.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe