Vinicius Junior Anajiandaa Kurejea Dimbani

Nyota wa Real Madrid Vinicius Junior anatarajiwa kurejea hivi karibuni baada ya kupambana na virusi vya corona.

Real Madrid ni miungoni mwa klabu zilizopata pigo la virusi vya Corona hivi karibuni, huku sehemu kubwa ya kikosi chake ikilazimika kuwa nje. Kwa sasa wachezaji wameendelea kurejea taratibu.

Marco Ansensio, Rodyrgo na Luka Modric waliweza kurejea kwa wakati kushiriki mechi iliyopita Real waliyopoteza dhidi ya Getafe.

Vinicius hakuweza kuwa tayari kuwa uwanjani na wenzake, kwa kuwa yeye alipatikana na maambukizi baada ya wenzie, hivyo kwa sasa anaripotiwa kuendelea vizuri na atarejea dimbani hivi karibuni.

Kwa mujibu wa chapisho la COPE,  Vinicius Junior tayari ameshapima na kupatikana bila maambukizi, na tayari ripoti ya vipimo yake imewasilishwa La Liga. Hata hivyo, staa huyu atalazimika kutumia takribani siku saba za kujitenga kwa mujibu wa sheria za serikali.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe