Katika soka kila kipindi huwa na historia yake ambayo kwa namna fulani huwa imejengwa ndani ya wachezaji ambao ndiyo hubeba falsafa nzima ya soka. Katika siku za karibuni baadhi ya nyota wa mchezo wa soka wamekuwa wakiibuka na kuonesha uwezo wao wa hali ya juu sana na kuzifanya baadhi ya timu kupishana kuwafukuzia ili kupata huduma zao.
Huu unaweza kuwa mwaka mzuri kwa raia wa taifa la Uingereza ambao kwa hakika wamekuwa na msimu mzuri sana na wenye mafanikio makubwa kwao. Wachezaji kama Jadon Sancho na Declan Rice ni kizazi ambacho taifa hilo linawahitaji na hakika wamekuwa na thamani ya aina yake katika soka hata pale watakapoamua kuzihama klabu zao hizo watauzwa kwa thamani ya pekee sana.
Jadon Sancho, nyota huyu ambaye aliachana na Manchester City na kuamua kujiunga na Borussia amekuwa na msimu mzuri sana huku akizama golini kwa kufunga mara 11 na kutoa pasi za magoli 17. Thamani yake imepanda hadi kufikia €150.3 milioni kwa klabu itakayomhitaji.
Matteo Guendouzi, akiwa amesajiliwa kutoka Lorient alisajiliwa na Arsene Wenger kutokana na uwezo wake wa kuchezesha timu jambo ambalo Wenger alishindwa kulifumbia macho kabisa. Kwa sasa thamani ya nyota huyo imepanda hadi kufikia €70.1 milioni huku akiwa tayari amecheza mechi 44.
Nicolo Zaniolo, klabu ya AS Roma inajivunia kuwa na aina ya wachezaji wa aina hii ndani ya kikosi chao ambao umri wao bado unawaruhusu kufanya makubwa hata baadaye. Kutokana na uwezo wake tayari amepanda thamani na kushika mioyo ya Wanaroma. Thamani yake imefikia €67.4 milioni.
Kai Havertz, nyota wa Bayer Leverkusen ambaye amekuwa na msimu wa pekee sana ndani ya kikosi chake. Akiwa tayari amefunga magoli 15 na pasi za magoli nne katika mechi zake 32 alizocheza ndani ya Bundesliga. Hadi sasa thamani yake imepanda hadi €64.3 milioni. Kutokana na uwezo wake aliwavuta Munich kutenga dau la €100 milioni.
Declan Rice, awali kabisa aliuteka moyo wa kocha wa taifa wa Uingereza, Southgate kwa kumuomba ahame kuchezea timu ya taifa ya Ireland na ajiunge na upande wa timu yao. Umri wake na mambo anayoyafanya yanaonesha ana mwangaza wa kufanya makubwa sana hapo mbeleni. Thamani yake hadi sasa ni €64.2 milioni.
Nyota wengine walio chini ya umri huo wanaotazamiwa kufanya vizuri na wakiwa tayari na thamani kubwa hadi sasa ni Gianluigi Donnarumma mwenye thamani ya €59.4 milioni, Vinicius Jr. mwenye thamani ya €55 milioni, Justin Kluivert mwenye thamani ya €44.3 milioni, Evan N’Dicka mwenye thamani ya €44.1milioni na Ryan Sessegnon mwenye thamani ya €43 milioni. Wote hawa wanahitaji dau kubwa sana ili kuwasajili wakiwa bado katika umri wa kawaida sana.


Fatina mfingi
Asnteh kwa taarifa meridianbet
Zeiyana
Soka limeendelea sana upande wa pili kwa wenzetu