Rooney Awaonya United Wasisajili Wazee!

Wayne Rooney ameibuka na kuwachana klabu ya Manchester United kuwa wasipagawe na kukimbilia kusajili wachezaji wenye majina makubwa ambo umri wao umeshaenda kama Cristiano Ronaldo au Gareth Bale akihofia kuwa klabu hiyo itatumia gharama kubwa mno.

United wapo katika kipindi ambacho maboresho yanahitajika kwa kiasi kikubwa ili kuongeza chachu ya kupambana vilivyo msimu ujao wakiwa chini ya uongozi mpya wa Ole Gunnar Solskjaer.

Wachezaji kadhaa wa Mashetani Wekundu wapo katika rada za uhamisho na inaaminika huenda msimu ujao usiwakute klabuni hapo akiwemo nyota Paul Pogba anayehusishwa zaidi na Real Madrid.

Manchester United wanahiji kikosi ambacho kitaweza kupambana vilivyo kwa kiwango cha juu kama wapinzani wao Manchester City ambao kwa sasa wamefanikiwa kuwa kutawala Ligi ya Primia wakati wao hawajaambulia hata kufuzu Ligi ya Mabingwa kwa msimu ujao.

Rooney, ambaye ana rekodi yake bomba ya kuchapa magoli klabuni hapo, anasema busara na subira ni vitu muhimu kwa klabu yake hiyoya zamani katika usajili ili kupata wachezaji bora vijana ambao watakuwa na mchango mkubwa wa mda mrefu klabuni hapo kuliko kuwachukua wachezaji wa gharama kubwa ambao umri umeshawatupa mkono.

“Kwa Ole (Gunnar) Kitu muhimu anachotakiwa kufanya ni kujaribu kujenga kikosi. Sidhani kama kumleta mchezaji mmoja au wawili kwa dau la zaidi ya paundi 100m itasaidia sana kwenye kikosi na kwa wachezaji ambao tayari wapo pale.” -Rooney

“unaweza kuwaleta wachezaji watatu, ukimleta Ronaldo, Sergio Ramos, na Lionel Messi au Gareth bale kwa mfano, itakugharimu Paundi 300-35m. Unapata miaka michache kwa Ronaldo, michache kwa Ramos na umetumia pesa nyingi.” -Rooney

Rooney anaamini huu ni wakati wa Manchester United kutumia Fursa ya Usajili kuingiza nguvu mpya ya vijana ambao damu bado inachemka kwenye kikosi na watatumika kwa mda mrefu.

2 Komentara

    Rooney mwamba ushaur mzuri

    Jibu

    Ni sahih

    Jibu

Acha ujumbe