Chelsea wamechomoa Ofa ya Juve kwa Emerson

Chelsea wanaripotiwa kuwa wamechomoa ofa ya klabu ya Juventus kwa Emerson Palmieri. Juve walikuwa wanamtaka staa huyu, lakini Chelsea wanahofia kuwa watakosa mbadala wake!

Ikumbukwe kuwa Meneja wa klabu hii pia, Maurizio Sarri anasaibni mkataba na klabu hii ya Juventus baada ya kusistisha mkataba wake na Chelsea kwa makubaliano maalumu.

Bila shaka meneja huyu angependa kuungana na Emerson ambaye amefanya poa sana kwa miezi ya hivi karibuni klabuni hapo kwenye safari yake kuelekea Serie A. kwa mujibu wa Calciomercato, Jue walitoa ofa yao ya mwanzo kabisa kwa staa huyu anayecheza nafasi ya beki wa kushoto, lakini ofa yao imebuma.

Hitaji la Juve limekuwa gumu kufanikiwa kwa sababu ya adhabu ya Chelsea juu ya kujhihusisha na usajili waliyopata kwa sababu ya kukiuka taratibu za usajili. Chelsea wanahitaji kushinda rufaa yao ya adhabu ya kutojihusisha na usajili ili waweze kuwa huru zaidi kwenye soko la usajili msimu huu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.