Akiwa ametimkia kwa miamba wa soka wa Hispania, Real Madrid ambao atakuwa akiwapa huduma msimu ujao kwa hakika atakuwa msaada sana ndani ya kikosi hicho na ni kama nafasi iliandaliwa kwa ajili yake na kila atakalofanya litakuwa na manufaa kutokana na uwezo wake mkubwa.
Alianza kuihudumia timu yake ya taifa akiwa na umri wa miaka 17, kati ya vitu vya pekee kwake ni kuanza kutumikia kikosi cha timu ya taifa akiwa na umri wa pekee sana ambao kwa hakika sio rahisi kwa wachezaji wengi kuanza kuaminiwa. Mwaka 2008 alijiunga rasmi na kikosi cha timu ya taifa ya Ubelgiji akiwa chini ya kocha René Vandereycken wakati wa mechi dhidi ya Luxembourg.
Aliwahi kutabiri nafasi za baadhi ya timu kwenye kombe la dunia, miongoni mwa vitu ambavyo aliwashangaza wengi ni kuchagua timu ambazo zilifuzu kwenye kombe la dunia lililofanyika Urusi. Baadhi ya timu hizo ni Ufaransa, Ubelgiji, Uingereza na Argentina. Aliposhindwa ni upande wa Argentina tu ambao alishindwa kwa kuwapa nafasi hiyo.
Ni shabiki mkubwa wa Zidane, safari yake hiyo kwake ni kama amekutana na mtu ambaye kwa miaka mingi alikuwa anatamani kuwa mbele ya macho yake. Zidane alikuwa ni mchezaji ambaye kwa wakati wote alikuwa akifuatiliwa na wengi ila Hazard yeye aliweka wazi kwamba mchezaji huyo wa zamani ana kiwango cha pekee sana na ujuzi uliokithiri ambao wengi wamejifunza.
Ni shabiki mkubwa wa mpira wa kikapu husasani New York Knicks, amekuwa akihudhuria mechi kadhaa za klabu hiyo na wakati mwingi amekuwa akijihusisha hata kushinda na mashabiki wenzake kuwapa nguvu wachezaji wao. Kwake hiyo ni nafasi kubwa sana na ni furaha kuthamini klabu yake hiyo pendwa.
Baba yake na mama yake pia walikuwa ni wanasoka, damu yao sio ya kutoka kwa mmoja pekee; wazazi wa nyota huyo ni wanamichezo wa miaka mingi na wote wawili wamekuwa wakijihusisha na soka miaka ya nyuma. Baba yake amechezea klabu ya Belgian Second Division akiwa kama mwanasoka mkubwa aliyejenga heshima ndani ya ligi hiyo kwa kipindi chake chote.
Namba yake ya jezi ni 10, anapendelea sana namba hiyo ya jezi ambayo ni namba ya historia kubwa sana kwake. Alipotua Chelsea alikuwa anavaa jezi namba 17 baada ya namba yake kuwa inatumiwa na Mata. Lakini baada ya kipindi fulani akairithi namba hiyo hadi sasa.

