Vinicius Jr Aigomea Jezi Namba 7

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ndani ya Real Madrid vinadai winga hatari ndani ya klabu hiyo Vinicius Jr inasemekana amepanga kugomea kuvaa jezi namba 7 msimu ujao ndani ya klabu hiyo.

Winga Vinicius Jr anaonekana kama mtu sahihi ambaye anatakiwa kuvaa jezi hiyo kwenye klabu ya Real Madrid na hiyo ni kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha ndani ya timu hiyo, Hivo klabu inaelezwa imempendekeza winga huyo wa kimataifa wa Brazil kuvaa jezi namba 7.Vinicius JrJezi namba 7 ndani ya klabu ya Real Madrid kwasasa inavaliwa na winga wa zamani wa Chelsea Eden Hazard ambaye hapati nafasi ya kucheza ndani ya timu hiyo kutokana na majeraha ya mara kwa mara, Hivo Winga wa Kibrazil ndio anapigiwa chapuo kuvaa jezi hiyo kwani Hazard anawreza kuachwa mwishoni mwa msimu huu.

Jezi namba 7 ndani ya Real Madrid ni jezi yenye heshima kubwa sana kwenye klabu hiyo kubwa zaidi ulimwenguni, Kwani imepita kwa magwiji wakubwa kwenye timu hiyo kama Raul Gonzalez Blanco na Crstiano Ronaldo hivo ni jezi kubwa yenye historia kubwa sana klabuni hapo jambo ambalo huenda linamuogopesha Vinicius Jr.Vinicius JrWinga Vinicius Jr amekua na muendelezo wa kiwango bora sana ndani ya klabu hiyo kwa misimu takribani mitatu sasa, Hivo klabu ya Real Madrid inaona ni wakati sahihi wa kimkabidhi jezi hiyo ambayo hua ni kama nenmbo ya klabu winga huyo ambaye inaonekana anaihofia jezi hiyo namba 7.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.