Vilabu vya ligi kuu vimekuwa vikihaha baada ya ligi kusimamishwa mwezi Machi kwasababu ya COVID 19, na pesa hiyo itaenda kusaidia kulipa mishahara ya wachezaji na makocha kipindi hiki ligi imesimama.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa TPLB, Stephen Mguto, pesa tayri imepelekwa kwenye akaunti za vilabu.
“Tunatoa shukrani kwa wadhamini wetu kwa kutupatia kiasi hicho pesa kama ilivyo kwenye makubaliano ya mktaba. Waliitoa pesa hii mapema kidogo lakini kulikuwa na ucheleweshwaji kidogo ndio maana imetoka wakati huu.
“Ni imani yetu pesa hii itasaidia vilabu kutatua changamoto walizokuwa nazo hasa kipindi hiki ligi imesimamishwa.”
Mguto pia amesema kiasi kilichobaki kitatolewa pna wadhamini pale ligi itakapoendelea.
Ligi kuu ya Tanzanian inaweza kuanza hivi karibuni baada ya Raisi John Pombe Magufuli kugusia kuhusu kurejea wiki iliyopita.
Katibu Mkuu wa Ndada FC, Seleman Kacheche amethibitisha kupokea msaada kutoka TPLB, amesema itasaidia kulipa mishahara hasa ya wachezaji.

“Angalau kiasi hiki kitasaidia kulipa mishahara wachezaji wetu ni moja ya matumizi yetu japokuwa haitoshi kukidhi mahitaji yetu yote.”
Juma lililopita, vilabu vingi vya Ligi Kuu viliomba msaada wa kifedha kutoka kwa TPLB ili kusaidia kipindi hiki cha Corona.
Vinara kwenye msimamo wa Ligi Simaba SC ni moja ya vilabu vichache ambavyo vina uwezo kiuchumi, kwani ina wadhamini lakini pia wanapata misaada kutoka kwa wanachama.


Fatina
Tunashukur kwa taarifa
Dorophina
Tunashukuru kwa taarifa meridian mpo juu
aisha
ahsanteni meridian kwa habari moto moto
Zeiyana iddi
Tunashukuru kwa taarifa meridianbet
Gabriel
Habari nzur
Ester mmakasa
Hongera TPLB kwa kujali vilabu .
mathayo sonje
ni jambo la msingi sana wamefanya bodi ya ligi maana ingekua ni shida kama kila timu ingejitegemea
Lydia Emmanuel Magoti
Habari nzuri
winfrida
inapendeza kwakweli kutoa ni moyo sio utajiri
Povel
Ni habar njema kwa vilabu vya bongo maana dah ilijanga limeathir timu nyng Sana hapa bongo Asante meridian kwa habar
felister
ni habari nzuri kwa vilabu maana itasaidia kuwalipa wachezaji mishahara yao
aisha
ahsanteni meridian kwa habari moto moto
Lombo
inapendeza iyo
Adelta
Habar nzuri meridian