Wolves Wamtimua Kocha O'neil

Klabu ya Wolves imemfuta kazi kocha wake Gary O’neil mapema leo baada ya muendelezo mbaya wa klabu hiyo kunako ligi kuu ya Uingereza wakiwa kwenye nafasi mbaya kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Baada ya kua na muendelezo huo wa matokeo mabaya klabu hiyo imeona moja ya suluhisho kwasasa ni kuachana na kocha wake Gary O’neil ambaye ameiogoza klabu hiyo toka mwaka 2023 akitokea klabu ya Bournamouth, Kwasasa klabu ya Wolves inatafuta kocha mpya ambaye ataweza kuwarudisha kwenye nafasi nzuri kuelekea mzunguko wa pili wa ligi kuu.wolvesMsimu uliomalizika klabu hiyo haikua kwenye wakati mgumu kama ambao unapitia sasa na kocha O’neil ndio alikua anaifundisha timu hiyo lakini mambo yameonekana kubadilika ghafla, Uamuzi wa klabu mpaka sasa umeangalia zaidi maslahi ya timu kwani haikua inaonekana klabu hiyo kurejea kwenye ubora chini ya kocha O’neil.

Mpaka sasa Wolves inashika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama 9 pekee baada ya kucheza michezo 16, Wakiwa wameshinda michezo miwili pekee wakipoteza michezo 11 na kutoa sare michezo mitatu pekee ikiwa ni wastani mbaya kwelikweli kwa timu ambayo inahitaji kuendelea kubaki ligi kuu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.