SIMBA YACHUKUA ZOTE TATU KWA MKAPA

Klabu ya Simba imefanikiwa kunyakua alama zote tatu kwenye mchezo wake wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya klabu ya CS Sfaxien kutoka nchini Tunisia baada ya kuicharaza mabao mawili kwa moja.

Simba kipindi cha kwanza mnamo dakika ya 3 tu waliruhusu bao baada ya beki wake wa kati Che Malone Fondoh kupiga pasi fupi ambayo ilinaswa na Hassen na kuweka mpira wavuni, Lakini wekundu wa msimbazi walitulia na kurejea mchezoni kuhakikisha wanasawaazisha na pengine kupata ushindi ndipo dakika ya 7 ya mchezo Kibu Denis akasawazisha na ubao kusoma 1-1.simba

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika wekundu wa msimbazi walikua wana umiliki wa mpira kwa asilimia kubwa na kutengeneza nafasi mara kadhaa za kufunga lakini hawakufanikiwa na mchezo huo kwenda mapumziko kwa sare ya bao moja kwa moja, Ambapo wapinzani wao muda mwingi wa mchezo wakionekana kua nyuma na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kuendelea walipoishia ambapo waliendelea kuutawala mchezo kwa kiwango kikubwa lakini awamu hii Sfaxien nao hawakua nyuma sana kwani walikua wakifanya majaribio ya kufika langoni kwa mnyama mara kadhaa, Lakini milango yote ilionekana kuendelea kua migumu.simbaKauli ya kwa Mkapa hatoki mtu ilidhihirika kwenye mchezo huu kwani mpaka dakika 90 za kawaida zilipomalizika ubao ulikua unasomeka 1-1, Lakini hali ilikua tofauti ambapo kwenye dakika ya 99 kwenye zile za nyongeza Kibu Denis aliipatia Simba bao la pili na kufanya waondoke na alama zote tatu na kufikisha alama sita kwenye kundi lao wakiendelea kushika nafasi ya pili.

Acha ujumbe