Simba Msituni Kuziwinda Alama Tatu Muhimu Leo

Klabu ya Simba leo inaingia vitani kuhakikisha inapata alama zote tatu leo dhidi ya klabu ya CS Sfaxien kutoka nchini Tunisia kwenye mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Simba wanazihitaji alama tatu za leo kwa udi na uvumba kwakua wanajua zitawaweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika, Kwnai wakiwafanikiwa kukusanya alama zote leo watafikisha jumla ya alama sita hivo watakua na alama tisa za kuzipambania katika michezo mitatu iliyobaki na kufanya kazi isiwe ngumu zaidi.simbaWekundu wa Msimbazi kama ilivyokua kawaida yao mara nyingi wanapokua kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa wamekua wakipata matokeo mazuri na leo wanawakaribisha Watunisia kwenye uwanja huo ambao timu nyingi vigogo wamewahi kucheza hapo na kuambulia vichapo, Hii ikiwa ni dalili nzuri kwa klabu hiyo yenye rekodi nzuri kwenye michuano ya Afrika.

Klabu ya CS Sfaxien mpaka sasa inashika mkia kwenye kundi ambapo wamecheza michezo miwili na kupoteza michezo yote na leo wanacheza ma klabu ya Simba ambao wamepoteza mchezo mmoja na kushinda mmoja, Hivo ni mchezo muhimu kwa timu zote Sfaxien wanaioana kama nafasi ya kufufua matumaini huku wekundu wa msimbazi wenyewe wakiona nao ni mchezo ambao unaweza kuwafanya kukaa kwenye nafasi nzuri ya kufuzu.

Acha ujumbe