Xavi Aanza na Ushindi Barcelona.

Meneja mpya wa Barcelona, Xavi Hernandez ameanza vyema baada ya kuongoza kikosi hicho kupata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Espanyol uwanjani Camp Nou.

 

Barcelona waliponea chupuchupu katika mechi hiyo iliyoshuhudia wageni Espanyol wakipoteza nafasi nyingi za kufunga mabao katika kipindi cha pili.

Bao la pekee na la ushindi kwa upande wa Barcelona lilipachikwa wavuni na Memphis Depay kupitia penalti ya dakika ya 48.

Ushindi wa Barcelona umewaweka katika nafasi ya sita kwa alama 20, nane nyuma ya Sevilla na Real Sociedad walio kileleni mwa jedwali.

Xavi alichezea Barcelona mechi 767 na akawaongoza kutia kapuni mataji 25 katika kipindi cha miaka 17. Hadi aliporejea Uhispania kuinoa Barcelona, Xavi alikuwa akinoa kikosi cha Al Sadd nchini Qatar.

Barcelona watavaana na Benfica ya Ureno ugani Camp Nou katika mchuano ujao wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA). Ushindi utawakatia tiketi ya kuingia hatua ya 16-bora ya kivumbi hicho.


WIKI NJEMA NA CRAZY TIME CASINO!

Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.