Mashabiki wa Fiorentina wametoa heshima kwa Stefano Pioli na Davide Astori baada ya dakika 13 kwenye mechi ya Fiorentina dhidi ya Milan.
Mashabiki hawa wa Fiorentina huwa wanamkumbuka aliyekuwa mlinzi wao na kapteni. Hii hutokea katika dakika 13, wakati huu ilikuwa ni namba ya jezi ya Astori.
Wakati huu waliamua kufanya kwa namna ya kipekee, wakipiga makofi na kuimba jina lake.
Pia, walitoa heshima kwa kocha wa Milan, Stefano Pioli ambaye alikuwa kocha wao wakati Astori alipofariki akiwa amelala Machi 2018, kabla ya mechi yao ya Serie A dhidi ya Udinese.

Sauti kutoka kwa umati wa mashabiki wa Fiorentina zilisikika zikisema ‘Pioli uno di noi’ huku wakipiga makofi, wakimaanisha kuwa ‘Pioli ni mmoja wetu’ wakati huo kocha huyu akiwa anatoa maelekezo kwa wachezaji wake wa Milan.
Stefano alikuwa kocha wa Fiorentina kwa misimu miwili na nusu, akishinda mechi 27 kati ya 74 akiwa Florence. Alichaguliwa kuwa kocha wa Milan mwaka 2019 baada ya kutimuliwa kwa Marco Giampaolo.
Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.


