Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane na kocha wa Barca, Koeman kwa wakati tofauti wamtuma pongezi zao kwa Atletico Madrid baada ya kutangazwa mabingwa wa kombe hilo baada ya miaka 6 bila kufanya hivyo!
Katika moja ya ligi zilizokuwa na wakati mgumu kutambua bingwa basi La Liga ni moja ya ligi hizo, kulikuwa na vita kali kati ya timu za juu, Atletico Madrid, Barcelona na Real Madrid.
Hata siku ya jana bado mbio za ubingwa huo zilikuwa kwenye meza. Real Madrid walihitaji kuwaombea mabaya Atleti ili waweze kushinda taji hilo,lakini Correa na Suarez walihakikisha kuwa Atletico Madrid wanashinda na kunyakua taji.
Baada ya ushindi huo, Zidane alitoa pongezi kwa Diego Simeone n akusema kuwa alistahili kushinda taji hilo kutokana na kukaa juu kwa muda mrefu. Kwa upande wa pili Koeman ambaye mbio zake za ubingwa ziliisha mapema sana apigwe na Celta Vigo.
Zidane alikipongeza kikosi chake kwa kufanikiwa kushinda mechi licha ya kuongozwa kwa 1-0 kabla ya kupindua matokeo baadae. Simeone amekuwa na Atleti kwa muda sasa na hilo ndio linalodaiwa kuwa chanzo cha mafanikio.
Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.
Safii
Nice update
Habari moto moto
Nice update