Kiungo mshambuliaji Raia wa Denmark ambaye anakipiga katika klabu ya Manchester United Christian Eriksen, ameonesha takwimu nzuri na kuvutia zaidi kutokana na uwezo wake wa kukimbia umbali mrefu kwa muda mchache.

Kwa mujibu wa mtandao wa UtdArena imetoa takwimu za Eriksen kwenye mechi ya Leicester City dhidi ya Manchester United kuwa, mchezaji huyo ameweka rekodi ya kukimbia umbali wa 10.69km kwa dakika 90 na hii inamfanya kuwa mchezaji pekee kwenye klabu hiyo kufanya hivyo kwa msimu huu 2022/2023.

Matokeo ya ushindi kwenye mchezo wa jana unaifanya Utd kusogea mpaka nafasi ya 5 kwenye msimamo wa Ligi kwa alama 9, na mechi inayofuatia ni dhidi ya Arsenal siku ya Jumapili waliopo nafasi ya kwanza kwenye Ligi kwa jumla ya alama 15.

Mara ya mwisho kukutana timu hizo, Manchester United walipoteza kwa bao 3-1.


